WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amewataka wadau wa miradi inayohusiana na usimamizi wa rasilimali za bahari kuwa walinzi ili kukabiliana na watu wanaofanya uvuvi haramu ili kutoathiri viumbe kwenye bahari.
Ndaki ameyasema hayo Wilayani Bagamoyo wakati makabidhiano ya majengo ya ofisi za vikundi vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi (BMU) kwenye soko la samaki Bagamoyo.
Alisema kuwa serikali imetenga fedha hizo ambazo zitatumika kununua boti 250 na kupitia mradi mwingine zitanunuliwa boti 70 ambapo wavuvi watakopeshwa ili waondokane na zana duni za uvuvi ili kuongeza uvuaji, kipato na lishe.
Naye Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amesema kuwa wadau hao wanapaswa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na uvuvi haramu kwani hiyo ni rasilimali muhimu inayopaswa kulindwa kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo.
Kwa upande wake mwakilishi wa katibu mkuu wa Wizara hiyo Steven Lukanga amesema kuwa malengo ya ujenzi wa Masoko ya samaki kwenye Wilaya tano za Mkinga, Bagamoyo, Lindi Vijijini na Tanga Mjini ni kuboresha uvuvi wa samaki ambapo kuna vikundi 50.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Abdala amesema kuwa wilaya hiyo inategemea mapato kutokana na uvuvi ambapo asilimia 30 ya mapato yanatokana na uvuvi na wameipa kipaumbele sekta ya Uvuvi ili kuboresha upatikanaji wa mapato na watakabiliana na uvuvi haramu ili kutoathiri mazao ya samaki. Jengo hilo la soko la samaki limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5
0 Comments