Header Ads Widget

MOTO WATEKETEZA BWENI SHULE YA MSINGI YA WAVULANA CHALINZE

 


MOTO ambao chanzo chake bado kufahamika umeunguza bweni la shule ya Msingi ya Wavulana ya Chalinze Modern Isalmic iliyopo Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alipotembelea shule hiyo iliyopo Chalinze Mzee kutoa pole na kujionea madhara ya moto huo ambapo haujaleta madhara ya kimwili kwa mwanafunzi yoyote.



Kunenge amesema alisema kuwa tukio lilitokea leo alfajiri  wakati wanafunzi hao wakiwa kwenye ibada Msikitini ambapo hakuna mwanafunzi aliyepata madhara licha ya baadhi ya vifaa kuteketea kwa moto huo.


Amesema kuwa hakuna wanafunzi walioumia na hakuna madhara ya kuzuru mwili na wataendelea na masomo kama kawaida na kuutarifu umma kuwa shule hiyo imepata changamoto ya tukio la Moto lakini wanamshukuru Mwenyezi Mungu haujaleta madhara ya mwili.


"Vitu zikiwemo sare, mabegi, sabuni, na baadhi ya madaftari walivyokuwa wakikaa navyo kwenye Bweni ndivyo vimeteketea kwa moto na hakuna mwanafunzi atakae kosa masomo kwa kosa sare na shule hiyo ni kubwa wanafunzi ambao bweni lao limeungua wamepata mahali pengine pa kulala na wataalamu tayari wameongea na vijana hao kuwatoa hofu na kuwashauri,"amesema Kunenge.


Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Pwani Jenipher Shirima ameeleza kuwa moto huo umefanikiwa kudhibitiwa mapema kupitia vizimia Moto vilivyopo shuleni hapo.


Shirima amesema kuwa kutokana na Changamoto ya moto mashuleni wapo kwenye Program ya utoaji mafunzo ambapo kila siku kuna shule ya msingi na sekondari Mkoani hapo inapatiwa mafunzo. 


Mkurugenzi wa Chalinze Modern Islamic Primary School Omary Ismail amesema kuwa bweni liloathirika ni la wavulana na vifaa vya wavulana nane ndiyo viliteketea vyote.

Ismail alishukuru kwa mafunzo ya Jeshi la zimamoto kwani vimewawezesha kuzima moto huo kwa muda mfupi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI