Header Ads Widget

BARABARA ZENYE UREFU WA KM 1176 KILIMANJARO KUTENGENEZWA

 


Na Gift Mongi, Moshi


Barabara zenye jumla ya urefu wa kilomita 1176 katika mkoa wa Kilimanjaro zinatarajiwa matengenezo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 na wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) ambapo jumla ya gharama shilingi bilioni 31.06.


Mhandisi Nicholous Fransis ni meneja wa TARURA mkoa wa Kilimanjaro ambapo alisema miradi ambayo itatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mwaka huo itakuwa ni 65  ambapo mwaka 2021/2022 jumla ya miradi 70 ilitekelezwa.


Alisema katika miradi ambayo ilikuwa ilitekelezwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa imeshakamilika kwa asilimia zaidi ya 80 ambapo kwa ujumla wake iligharimu kiasi cha bilioni 22.6.


"Hadi tunapoenda kumaliza huu mwaka wa fedha ni kuwa miradi yote ambayo ilikuwa katika utekelezwaji itakuwa imeshakamilika kama ambavyo tulikubaliana na wakandarasi wapo katika maeneo yao wakikamilisha"alisema


Alisema katika kipindi hicho miradi ya barabara za changarawe ilikuwa ni kilomita 1318 wakati zilizowekewa changarawe kwa upya ni kilomita 312 pamoja na za lami kilomita 12


Kwa mujibu wa mhandisi Nicholous ni kuwa kwa mwaka ujao wa fedha  fedha hizo ambazo zitakuwa zimeongezeka tofauti na mwaka huu unaoishia vyanzo vyake ni pamoja na kutoka mfuko wa barabara,ongezeko kutoka mfuko wa majimbo sanjari na fedha za tozo.


Alisema hadi kufikia katikati ya mwezi ujao taratibu za manunuzi zitakuwa zimeshaanza ikiwa ni pamoja na kutangaza tenda kwa ajili ya kuwapata wakandarasi ili utekelezaji uweze kuanza mara moja.


"Mwenge wa uhuru ulivyopita jumla ya miradi 6 ya barabara iliwekwa mawe ya msingi au kuzinduliwa  katika wilaya zote za mkoa na miradi hiyo mitano ilikuwa kwa kiwango cha lami na mmoja uliopo kule Same ni wa kiwango cha changarawe"alisema


Diwani wa kata ya Mwika Kaskazini Samwel Shao alipendekeza wakandarasi wanaopewa miradi hiyo kuitekeleza kwa wakati kabla mvua hazijaanza kwani mara nyingi kumekuwepo na kero barabara kuchongwa na kisha mkandarasi kupotea na kuwaacha wananchi wakipata adha ya kupita.


Alisema ipo haja ya TARURA kuangalia upya utaratibu wa kumpa mkandarasi mmoja miradi mingi kwani anashindwa kuitekeleza kwa wakati na kusababisha malengo ya serikali katika kuwatea wananchi maendeleo kutotimia.


"TARURA wasimfumbie macho mkandarasi ambaye ataonekana ni mzembe kwani hawa ndio wanaoichonganisha serikali na wananchi kama hana vifaa ni bora aache mwenye navyo ili hio miradi na mipango ya serikali iweze kutimia"alisema


Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI