Header Ads Widget

MBUNGE ZUENA AIOMBA SERIKALI KULINUSURU ZIWA JIPE.

 



NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri ameitaka serikali kufanya hatua za haraka kuteketeza magugumaji katika ziwa Jipe lililopo wilayani Mwanga mkoani hapa ili kulinusuri kufa.


Kauli hiyo aliitoa jana ambapo alisema kuwa, ziwa Jipe lililopo katikati ya mpaka wa Tanzania na Kenya lakini limekuwa na magugumaji kiasi kwamba shughuli zote za uvuvi kwa upande wa Tanzania hazifanyiki.



"Ikumbukwe kwamba chanzo cha maji katika ziwa hili kinatoka katika mlima Kilimanjaro lakini upande wa wenzetu Kenya wametengeneza mazingira mazuri na miundombinu ya utalii wananufaika kupitia ziwa hili kwa upande wetu magugumaji yamezidi kiasi kwamba hata wakazi wa pale wameshindwa kuvua samaki" alisema Mbunge Zuena.


Mbunge huyo ameiomba Serikali iangalie kwa kina na kufanya haraka kuyaondoa magugumaji hayo kwa sababu ziwa hilo linalisha maji yake katika Bwawa la nyumba ya mungu ambalo hutumika kuzalisha umeme hali ambayo imepelekea kupungua kwa kina cha maji kutokana na kuathiriwa na magugumaji.



"Mradi wa Maji Same- Mwanga- Korogwe umetengewa fedha na mradi huo utachukua maji Bwawa la nyumba ya mungu ambayo chanzo chake ni ziwa Jipe kuendelea kwa magugumaji haya kutapelekea maji kukauka na mradi huo kukosa tija hivyo juhudi za haraka zinahitaji kuyateketeza magugumaji haya" alisema Mbunge Zuena.


Akizungumza swala la mikopo ya halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambao ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri alisema kuwa, mikopo hiyo imekuwa ikiwajenga kiuchumi makundi hayo.



Alisema kuwa, wakinamama wengi wamekuwa wakichukua mikopo hiyo na kufanya shughuli mbalimbali zinazowawezesha kulea familia na kusomesha watoto lakini changamoto iliyopo ni mikopo hiyo kutotosheleza uhitaji wake.


"Mikopo hii imekuwa haitoshi kwa sababu wanawake wengi wanaochukua mikopo hii na kwenda kuifanyia biashara wakirudisha wanakuta vikundi vipya vimejiunga na bado hela haitoshelezi hivyo niishauri Serikali kuachana na mtindo wa asilimia kumi na badala yake iwatafutie fedha wamachinga wakope" alisema Mbunge Zuena.


Akizungumzia swala la Bajeti ya mwaka 2022/2023 alisema kuwa bajeti hiyo imekonga mioyo ya Watanzania wote na kutumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hasani.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI