Header Ads Widget

UCSAF YAWAKUMBUKA WAGONJWA MIREMBE YATOA MSAADA WANYE THAMANI YA SH.MILIONI 3.5

 


 

Na Hamida Ramadhan Dodoma


MFUKO wa Mawasiliano kwa wote UCSAF umetoa msaada wa vyakula mbalimbali na maboksi ya taulo za kike katika Hospitali kuu ya Afya ya Akili Mirembe wenye Thamanni ya jumla ya Shilingi Milioni 3.5 


Akiongea leo Machi 22 2022 jijini hapa Mara baada ya kukabidhi msaada huo  Justina Mashiba Afisa Mtendaji Mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) amesema (UCSAF) ni Taassi ya Serikali na majukumu yao makubwa ni kupeleka mawasiliano vijijini.


Amesema wamekwenda kutoa msaada katika hospitali ya Mirembe na kuwasalimia wagonjwa waliopo hospitalini hapo Kama njia mojawapo ya kurudisha walichojaaliwa katika jamii.




"Hasa ukizingatia mwezi Machi ni mwezi wa wanawake na tumeadhimisha nakusherekea Siku ya wanawake hivyo tumeona ni busara kuleta kitu kidogo tulichonacho kwaajili ya kuwasaidia ndugu zetu waliopo hospitalini hapo wakipatiwa matibabu,"amesema Mashiba.


"Nakuongeza Kusema"Sisi kama wanawake tuliopo serikalini tumeona ni vizuri kutoa kidogo tulichonacho kwa ajili ya wenzetu hawa wanaopatiwa matibabu hospitalini hapa mirembe na yote ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa  kuweza kutuvusha salama na kuingia mwaka mpya na kusherekea katika maadhimisho ya Siku ya wanawake, kama tuliweza kufurahi basi na wezetu walioko hapa nawao waweze kufurahi,"amesema.


Naye Nadia Amir Muweka hazina UCSAF amesema wamefurahi kuwa hapo na kutoa kidogo walichopata kwaajili ya jamii hasa wagonjwa wanaopatiwa matibabu Hospitali ya mirembe Kama sehemu ya maadhimisho hayo.


" Nawapongeza Sana Uongozi wa hospitali ya Mirembe na Uongozi wa (UCSAF) kwa kushirikiana pamoja katika kuhakikisha Siku hiyo inafanikisha tunashukuru kuwa hapa na kutoa hiki tulichojaliwa.


Na kuongeza kuwa"Tumechagua mirembe tumeona hapa kunauhitaji Mkubwa lakini pia hapa ni nyumbani na UCSAF ipo Dodoma hivyo niseme wazi kutoka moyoni kama waafirika tunapitia maisha tofauti hivyo mtu akikosa tunakuja anavyojisikia kwa hiki kidogo tulichotoa tunajisikia ni wenye furaha," amesema Muweka Hazina Nadia


 


Naye Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya afya ya Akili Mirembe Dkt Paul Lawala amesema Wanashukuru kwa msaada wa Sukari ,Mafuta ,Maharage Mchele na taulo za kike wameonyesha ni jinsi gani wanawajali 


Kwa upande wake Katibu wa Afya  Hospitali ya Mirembe Jackson Mjinja amewashukuru UCSAF kuwapelekea  matendo hayo ya huruma na kuomba na watu wengine waguswe kupeleka misaada kamaa hiyo kwani huitaji ni Mkubwa hususani kwa wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akili.


Amesema Hospitali ya Mirembe imegawanyika katika sehemu  kuu nne, ambapo kuna Mirembe yenyewe  Hospitali kuu wagonjwa wakawaida eneo la Isanga wagonjwa Wa akili na wenye kesi 234, eneo la Itega  ni wagonjwa wa akili walioathirika na Madawa ya kulevya 524 ,Hombolo kilimo na ufugaji na waliotelekezwa na jamii wapo 6 lakini pia kuna eneo lao la Annex kwaajili ya miradi ya Hospitali.




"Tunatoa shukrani kwa mkurugenzi wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) na Hospitali ya Mirembe kwa mashirikianao mazuri na kuhakikisha  kuleta misaada hasa katika kusherehe yao Siku ya wanawake na kutukumbuka sisi Mirembe,"amesema Katibu Mjinja.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI