NA AMINA SAIDI, TANGA.
Tanzania Bara imepiga hatua kubwa katika Sekta ya maji kwa kuzindua rasmi Mwongozo wa uundaji na uendeshaji wa jumuia za watumia maji (WUAs).
Uzinduzi huo wa kihistoria umefanyika jijini Tanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wataalamu wa maji pamoja na wadau wa maendeleo kuonyesha dhamira ya nchi katika kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji safi na salama kwa wananchi wake
Aidha Mwongozo huo mpya unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika usimamizi wa Rasilimali za maji kwa kuiweka mfuko thabiti na bayana wa uundaji na uendeshaji wa jumuiya hizi muhimu.
Pia jumuiya za watumia maji ni vikundi vinavyongozwa na wananchi wenyewe vikipewa jukumu la kusimamia kuendesha na kutunza miundo mbinu ya maji katika maeneo yao na kuhakikisha uwajibikaji wa moja kwa moja.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo Naibu Karibu Mkuu Wizara ya Maji Agnes Meena amewaagiza Wakurugenzi wa Bodi za mabonde nchini kufanya tathmini ya hali ya jumuia zilizopo kwenye maeneo yao na kuwasilisha taarifa hiyo Wizarani kwa lengo la kujua ni jumuia gani zinafanya kazi vizuri na zipi zinahitaji kuwezeshwa kwa Namba moja au nyimgine.
Aidha alimesema anatambua changamoto kubwa za jumuia kukosa ufanisi ni kukosa fedha za kianzio na miradi ya kipato kwa jamii husika,miradi haitatumika kama motisha ili kuongeza upatikanaji wa kipato kwa jamii inayotekeleza shughuli za uhifadhi.
Amesema pia Wizara kw a kushirikiana na wadau mbali mbali inaendelea na jitihada za kuwajengea uwezo kwa jumuiya za watumia maji ili kuboresha ufanisi wake katika maeneo ya utunzaji wa maji.
Ninatambua kujenga uwezo ni suala endelevu hivyo Wizara inaendelea kushirikiana na wadau kuwajengea uwezo Taasisi zake ikiwemo jumuia ili kuhakikisha suala la usimamizi wa Rasilimali za maji linatekelezwa ipasavyo"alisisitiza Meena.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Rasilimali za maji kutoka Wizara ya Maji Rosemary Rwebugisa amesema Tanzania Bara ina jumla ya jumuia 201 ambapo Mwongozo huo umetayarishwa chini ya ufadhili wa Shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ )kupitia umoja wa Ulaya.
Mwongozo huu utasaidia kutoa dira kwa jumuiya zote za watumia maji kusimamia kwa umakini zaidi kuliko ambavyo ilikuwa ikifanyika wali Kila jumuiya ilikuwa ikiendesha shughuli bila kuwa na muongozo maalumu"alisema Rwebugisa.
Naye Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Bodi za maji za mabonde Tisa yaliyopo Tanzania Bara Mhandisi Segule Segule alisema Mwongozo huo una umuhimu mkubwa kwani unatoa mfuko utakao wawezesha kuendesha shughuli kwa pamoja.
Segule amesema Jumuiya na wadau wote kwa jumla wautumie Mwongozo huo Kama fursa muhimu utakaowawezesha kuendesha shughuli kwa pamoja badala ya Kila mmoja kivyake.
0 Comments