Header Ads Widget

JUKWAA LA VIJANA CHAMWINO LATAKA ONGEZEKO LA BAJETI YA ELIMU HALMASHAURI YA CHAMWINO

 




HALMASHAURI ya Chamwino imetakiwa kuongeza bajeti kwenye sekta  ya elimu ikiwa ni pamoja na  kutenga fedha  na kuongeza idadi za shule jumuishi ili kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum.


Akitoa mapendekezo ya jukwaa la Vijana Wilaya ya Chamwino,kuhusu maboresho katika sekta ya elimu,katika mkutano ulioandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la ActionAid Tanzania,Mjumbe wa Jukwaa hilo,Magreth Malongo amesema ili  kufikia lengo namba  4  la maendeleo endelevu ya dunia,pamoja na kutatua changamoto zilizopo  nguvu inahitajika katika ngazi ya Wilaya.


Amesema kuna haja ya Halmashauri hiyo kuongeza bajeti katika sekta ya elimu hasa katika madawati,nyumba za walimu na matundu ya vyoo kwani hali imekuwa sio nzuri katika Halmashauri hiyo yenye Majimbo mawili ya Mvumi na Chamwino.


“Sisi kama wanajamii tunapendekeza changamoto hizi   zitatuliwe  kupitia Mfuko wa bajeti wa Halmashauri ya Wilaya  na kuondoa msongamano wa wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa,’’amesema Malogo.


Kwa upande wake,Mwakilishi wa Jukwaa hilo,Mariam Mahajile amesema kutokana na kuongezeka idadi wa watoto wenye mahitaji Maalum  kuandikishwa kutoka watoto 35 mwaka 2015 hadi 61 mwaka 2021 walioko nje ya mfumo jukwaa hilo lilipendekeza Halmashauri   kutenga na kuongeza idadi za shule jumuishi ili kuwasaidia.


‘’Kutenga Bajeti kwaajili ya watu wenye mahitaji maalum  pamoja na kuongeza idadi ya walimu waliobobea kwenye taaluma hiyo kwani wanahitaji huduma za kutosha tofauti na wa kawaida,’’amesema Mahajile


Akipokea mapendekezo hayo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Edson Sweti  amesema wameyapokea mapendekezo hayo na kuahidi wataongeza bajeti hiyo huku akitoa maagizo kwa Maafisa Elimu kubaini walimu Maalumu ili waweze kwenda kwenye shule lengwa ili kupunguza uhaba huo.


‘’ Tunawalimu wa kutosha ambao tayari tushawapeleka kwa miaka mitano masomoni  tuwapeleke kwenye shule lengwa ili wakafanye kazi lengwa , maana mwaka jana katika mapato yetu tulikusudia kukusanya bilioni 2.1 mpaka sasa tumekusanya kwa asilimia 92 mwaka unaokuja tumeongeza kutoka bilioni 2.1 mpaka bilioni 3,’’amesema Sweti.


Mwakilishi wa Afisa Elimu Wilaya hiyo,Neema Milumbi amesema mapendekezo hayo yatawasaidia katika kusimamia, kufuatilia na kupanga  bajeti  kwa mwaka ujao  wa fedha.


‘’Wamezungumzia juu ya miradi ya jimbo , bajeti ni ndogo kama Milioni 98 au 99 lakini bajeti hiyo inagawanyika kwa majimbo mawili Mvumi na Chamwino bajeti hiyo ni finyu  sana,”amesema na kuongeza


“Kwahiyo ni vigumu sana kama walivyoshauri iende kwenye tarafa moja kwa sababu fedha zile zipo kwaajili ya kuchochea miradi ya maendeleo.’’amesema kaimu Afisa elimu huyo.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI