MCC Salim Faraj Abri Asas
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Diwani wa Kata ya Mkimbizi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Eliud Peter Mvela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Uchumi na Afya, ameweka wazi utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kata yake na kutoa shukrani kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Salim Faraj (ASAS), kwa mchango wake katika kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumza na Matukio Daima Media, Mvela ameeleza kuwa mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kata ya Mkimbizi, Manispaa ya Iringa, yanaendelea kuonekana kupitia miradi mbalimbali katika sekta za elimu, afya na miundombinu, na kusisitiza kuwa jitihada za serikali zimeongezewa nguvu na mchango wa wadau binafsi, akiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Salim Abri (ASAS), ambaye amekuwa miongoni mwa wanaoisaidia serikali katika kutekeleza miradi hiyo.
“Kipindi naingia katika uongozi wangu, moja ya changamoto kubwa ambayo niliikuta katika Kata ya Mkimbizi ni pamoja na eneo la Makaburi ya Igereke ambalo lilikuwa katika hali mbaya sana kwa sababu halikuwa na uzio, lakini pia hata vyoo vilivyokuwapo katika eneo hilo havikuwa katika hali nzuri.
Nilipoingia kwenye uongozi, ukarabati wa eneo hilo la makaburi ulikuwa ni ahadi yangu kwa wananchi na nichukue nafasi hii kuishukuru Kampuni ya ASAS pamoja na familia yake kwa kuchangia shilingi milioni 15 katika ujenzi wa uzio katika eneo la Makaburi ya Igereke.
Katika mchango huo wa ASAS, hakuna hata kiasi cha fedha ya serikali kilichotumika katika ujenzi wa uzio huo, ambapo fedha za serikali ziliendelea kutumika kusaidia miradi mingine ya maendeleo.”
Aidha, ameongeza kuwa suala la utoaji wa michango kwa ajili ya maendeleo halipaswi kuangaliwa kwa msingi wa utajiri bali moyo wa kujitolea na amewataka wadau na wawekezaji wengine kujitokeza kwa wingi kusaidia maendeleo ya miradi mbalimbali kama anavyofanya ASAS.
“Mimi niseme tu watu waige kile ambacho ASAS pamoja na familia yake wamekuwa wakikifanya kwa kujitoa kwa kiasi kikubwa kusaidia miradi ya maendeleo.
kuwa ukifuatilia kwa karibu si kwamba ASAS hana matumizi ya fedha anazotoa bali ni wito wa kujitolea ambao amekuwa akiutekeleza kwa nia ya kuisaidia serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.
Suala la utoaji halipaswi kuangaliwa kwa msingi wa utajiri ndiyo maana wale wanaotoa wanazidi kufanikiwa kwa sababu Mungu anazidi kuwaongezea.
Katika jamii wapo wadau na wawekezaji wengi mimi niwaombe tu wajitokeze pale wanapoona kuna uhitaji wa kuisaidia serikali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.”
Pia, Mvela ameimshukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa kiasi kisichopungua shilingi bilioni 2.66 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata ya Mkimbizi.
Aidha, amempongeza Rais kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo, huku akieleza kuwa kutokana na utendaji wake, anastahili kupewa muda mwingine ili kuendeleza jitihada hizo.
“Kikwelii katika utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata ya Mkimbizi isingewezekana kufanikiwa bila juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa kiasi kisichopungua shilingi bilioni 2.66 kwa ajili ya miradi mbalimbali katika kata yetu ya Mkimbizi, ambapo kiwango hicho ni nje ya kiasi kisichopungua shilingi bilioni 9 kinachotarajiwa kutekeleza mradi wa barabara ya kiwango cha lami, mradi ambao unatarajiwa kuanza mwezi Julai na utakuwa na urefu wa kilomita 4.
Aidha, Mvela amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumteua kuwa Diwani kupitia chama hicho, huku akieleza kuwa ameendelea kupata ushauri na miongozo muhimu iliyomwezesha kushughulikia matatizo mengi ya wananchi yaliyokuwepo tangu enzi za uhuru.
0 Comments