Header Ads Widget

SERIKALI YAENDELEA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATU WENYE ULEMAVU






Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu hassan imeendelea kutoa kipaumbele kwa Watu wenye Ulemavu kwa lengo la kukuza ustawi wa kundi hilo.

 

Amebainisha hayo  jana Machi 6, 2022 walipotembelea Kituo cha Watoto wenye Ulemavu kilichopo Shule ya Msingi Bwagira kwa lengo la kutoa msaada kwa Wahitaji mbalimbali ambapo Ofisi yake imeshirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga pamoja na Wadau ikiwa ni sehemu ya maadhimisho kuelekea Siku ya Wanawake.

 

Naibu Waziri Katambi alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Miongozo na Mikataba ya Kimataifa ili kuifanya jamii itambue umuhimu wa kuwahudumia Watu wenye Ulemavu sambamba na kutoa kipaumbele kwa kundi hilo katika nyanja mbalimbali.

 


“Serikali imeendelea kutunga Sheria, kuandaa miongozo na taratibu ili kuwezesha Watu wenye Ulemavu waweze kupata haki na stahiki za msingi ikiwemo elimu, huduma za kiafya, ushiriki katika masuala ya uchumi pamoja na kushirikishwa kwenye maeneo ambayo wao watajiona ni sehemu ya ujenzi wa Taifa lao,” alieleza Katambi

 

Aliongeza kuwa, Serikali hii inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa Watu wenye Ulemavu na ndio maana imeweka Wizara maalum ambayo inashughulikia masuala yao kwa ukaribu.

 

“Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan anawajali na kuwapenda sana wenzetu wenye Ulemavu, Vijana, Watoto, Wanawake na amekuwa akipaza sauti kwa ajili ya kupigania haki za makundi hayo,” alisema Naibu Waziri alisema

.

 


Sambamba na hayo, Naibu Waziri Katambi alipongeza jitihada za Wanawake katika Mkoa wa Shinyanga na maeneo mbalimbali kwa namna wanavyojitoa katika jamii zinazowazunguka na kusaidia watu wenye uhitaji.

 

“Kwa kweli jambo hili ni kubwa na nitaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana pamoja nanyi ili kuhakikisha wenye mahitaji wanapata haki zao,” alisema



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI