Na THABIT MADAI,ZANZIBAR
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Sada Mkuya Salum amewataka Waandishi wa Habari Nchini kuendelea kuibua Changamoto zinazowakabili Watu Wenye Ulemavu Mjini na Vijijini kwa lengo la kuwaondolea zinazowakabili katika Maisha yao ya Kil Siku.
Wito huo ameutoa leo Wakati akifungua Mafunzo ya Siku Mbili kwa Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari Nchini juu ya Kuandaa na kuandika Habari za Watu wenye Ulemavu ambapo Mafunzo hayo yamefanyika katika Hotel Maru Maru Mjini Unguja.
Waziri Sada alisema kuwa, Ofisi ya Makamu wa Kwanza ipo tayari kuwasaidia Wahitaji mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu hivyo Waandishi wa Habari wanatakiwa kuongeza nguvu zaidi katika kuibua changamato zinazowakabili.
“Waandishi wa Habari wamekuwa wakifanya kazi nzuri sana katika jamii ya kuibua changamoto mbalimbali zinazowakabili hivyo niendelee kuwaomba waongeze nguvu zaidi katika kuibua changamoto hizo ili Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimali tuweze kuwaondolea changamoto hizo,” alisema.
Pia alisema kuwa, hadi sasa tayari Serikali imeweka Mazingira wenzeshi kwa watu wenye ulemavu kuweza kupata haki na fursa sawa na Binadamu wengine.
Aidha Waziri Sada Mkuya amewataka Waandishi wa Habari kuwa Mstari wa mbele katika kushajihisha jamii kuweza kuwatoa Watu wenye ulemavu kuhesabiwa wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
“Kuelekea katika Sensa ya Watu na Makaazi ya mwaka 2022 sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha kuwa Watu wenye Ulemavu wote wanahesabiwa kwa lengo la kuwawezesha kupata fursa zao,”alieleza.
Nae Mratibu wa Miradi kutoka Internews Shabani Maganga alisema kwamba, lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea Uwezo na kuongeza Maarifa kwa Waandishi wa habari juu Watu wenye Ulemavu.
“Katika Mafunzo haya yatasaidia sana kuongezeana Maarifa, Ujuzi pamoja na uwelwa juu ya Watu wenye Ulemavu ili kusaidia kupata haki na fursa zao,”alieleza
Mafunzo hayo ya Siku Mbili ambayo yanawajumuisha Waandishi mbalimbali Unguja na Pemba huku mada mbalimbali zimewasilishwa katika Mafunzo hayo.
0 Comments