Header Ads Widget

WAZIRI SIMBACHAWENE AITAKA TAASAISI YATAIFA YA UTAFITI KUSAMBAZA DAWA ZA COVID-19 NCHINI


Na Hamida Ramadhan, Matukio. DaimaApp Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, ameitaka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kuhakikisha dawa zilizotengenezwa kwa ajili ya tiba au kinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 zinasambazwa kwa haraka katika maduka makubwa ya dawa ili ziweze kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Akiongea katika banda la tasisi hiyo katika wiki ya utumishi wa umma Dodoma waziri huyo amesema ni muhimu dawa hizo zipatikane kirahisi kwa wananchi kwa kuwa zilitokana na tafiti za kisayansi zilizofanyika nchini, hivyo ni hatua ya kuenzi jitihada za watafiti wazalendo na kuimarisha afya ya jamii.

“Tunataka kuona dawa hizi, ambazo zilithibitishwa kutibu au kuzuia Covid-19, zikipatikana katika maduka ya dawa makubwa kote nchini ili jamii iweze kunufaika moja kwa moja. Si vema zikabaki kwenye maabara au kwenye mipaka ya taasisi pekee,” alisema Waziri Simbachawene 

Akijibu agizo hilo, Mwakilishi kutoka NIMR, Dkt, Akili Kalinga mtafiti mwandamizi NIMR, alisema taasisi hiyo imepokea maelekezo ya Waziri kwa uzito mkubwa na tayari imeshaanza utekelezaji wa mkakati wa kuhakikisha dawa hizo zinasambazwa nchi nzima. Alisema mikoa ya Dar es Salaam tayari imeanza kupata dawa hizo kupitia maduka makubwa ya dawa, na mikoa mingine itaendelea kufikiwa.

“Tunaendelea na juhudi za kuhakikisha dawa hizi zinasambazwa kwa upana zaidi. Tayari tumeanza Dar es Salaam, na dhamira yetu ni kuhakikisha kila mkoa unazipata. Huu ni mkakati wa kitaifa na tunautekeleza kwa bidii,” alisema Dkt Kalinga

Dkt. aliongeza kuwa NIMR inaendelea kufanya tafiti mbalimbali kuhusu magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, magonjwa ya moyo, saratani, kifua kikuu, malaria, na magonjwa mapya ya mfumo wa upumuaji. Pia, taasisi hiyo imeweka mkazo katika utafiti wa dawa zinazotokana na mimea tiba ambazo zilitumika enzi za mababu.

“Tunatambua umuhimu wa tiba asilia. Kama taasisi ya utafiti, tumekuwa tukikusanya na kuchambua taarifa za kisayansi kuhusu mimea tiba, tukilenga kuimarisha mfumo wa afya unaotegemea rasilimali za ndani,” alisema Dkt Kalinga.

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ni taasisi chini ya Wizara ya Afya inayojihusisha na utafiti wa magonjwa mbalimbali kwa lengo la kusaidia serikali kuweka sera bora za afya na kutoa tiba sahihi kulingana na ushahidi wa kisayansi.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI