Na Amon Mtega,_Songea.
KOCHA wa timu ya Mbeya kwanza Maka Mwalisi amefurahishwa na uwanja wa michezo wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma kutokana na ubora wa kusakatia kabumbu.
Furaha ya uwanja huo ameipata baada ya timu yake ya Mbeya kwanza kuutumia kama uwanja wa Nyumbani ambapo katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya NBC timu hiyo imeanza kuutumia rasmi uwanja huo kwa kuvaana na watani wao Mbeya city ambao wote wanatokea jiji la Mbeya.
Kocha Mwalisi akiuzungumzia uwanja huo amesema kuwa licha ya mchezo wa Mbeya kwanza na Mbeya city kutoka sale ya kutokufungana lakini unaona viwango vya wachezaji wake wakitembea na mpira kutokana na uwanja kuwa mzuri.
Hata hivyo kocha Mwalisi amewashukuru wakazi wa Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kwa ushirikiano wanaonyesha katika kuishangalia timu ya Mbeya kwanza na kuwafanya wachezaji wa timu hiyo kuwa na moyo wa kujituma wakati wa kusakata kabumbu.
Kwa upande wake kocha wa timu ya Mbeya city Mathias Lule katika mchezo huo ameonekana kushangazwa na wachezaji wake kuwa wamecheza chini kiwango licha ya uwanja wa Majimaji kuwa bora kwa michezo na matokeo yake wametoka bila kufungana na kuambulia timu hizo kugawana alama ya moja moja.
0 Comments