Na,Jusline Marco:Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ametoa muda wa siku 30 kwa halmashauri ya Wilaya ya Meru kuhakikisha wanafuta vibali vya viwanja vilivyotolewa kinyemela katika eneo la hifadhi ya mto Usa.
Aidha Mhandisi Ruyango ameongeza kuwa halmashauri ya Meru imejipanga kuotesha Miti Milioni 1.5 na kuopongeza Bodi ya maji Bonde la Pangani kwa kuendelea kutoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Akizungumza kwenye zoezi la upandaji miti lililofanyika katika mto huo Wilayani Arumeru, Mhandisi Ruyango pia ameagiza kutolewa notis kwa wakulima waliolima mazao yao pembezoni mwa mto huo kuyaondoa ili kuacha eneo la mto huo kuwa salama.
Kwa upande wake Mwenye kiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Jeremia Kishili amesema kuwa maji ni uhai na maji hayana mbadala hivyo amesema halmashauri hiyo itahakikisha inasimamia vyanzo vyote vya maji vinajifadhiwa.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Nkoanekoli,Braham Nanyaro amesema zoezi la uoteshaji wa miti litaboresha ipatikanaji wa maji na utunzaji wa mazingira.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani,Muaidolojia Philipo Patrick amesema eneo ambalo wamelichagua kuotesha miti linachangamoto za uhifadhi ambapo amesema umbali wa mita 60 zipo kisheria na hazipaswa kuingiliwa kwa shughuli zozote zile.
0 Comments