Mkuu wa wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro Thomas Apson amewataka wananchi na wakazi wa wilaya ya Siha kutumia mitandao ya kijamii kwa kujinufaisha kiuchumi badala ya kutumia mitandao hiyo kueneza chuki kwa jamii.
Hayo ameyasema katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha wakati akitoa salamu katika Baraza maalum la Madiwani lililoitishwa kwa lengo la kupitia mapendekezo ya Bajeti ya RUWASA kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Amesema kuwa wapo baadhi ya watu wachache katika wilaya ya Siha wanatumia mitandao ya kijamii vibaya katika kutoa taarifa za kuchonganisha na kuleta sintofahamu katika jamii ya wanaSiha.
Ametoa wito kwa wale wote wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake watumie mitandao hiyo katika kujinufaisha kiuchumi pamoja na kuitangaza vema wilaya ya Siha ili iendelee kupaa zaidi kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.

Mwisho.
0 Comments