Header Ads Widget

DC MUFINDI APIGA MARUFUKU VIJANA KUKAA VIJIWENI,ASIFU MRADI WA YAM


SERIKALI ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa   imewataka vijana kupitia mradi  Youth Agency Mufindi (YAM) kuunda vikundi vya kiuchumi ili kunufaika na mikopo isiyo na riba toka Halmashauri badala ya kukaa Vijiweni bila kazi .

Rai hiyo ilitolewa jana na mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule wakati akizungumza na vijana 100 wanaotoka kwenye mazingira magumu kata za Ihanu ,Luhunga na Mdabulo wanaoendelea  na mafunzo ya Afya ya akili kwenye Ukumbi wa Yatima Igoda .

 Mtambule aliwataka vijana hao kuunda vikundi na wale wenye ulemavu kuungana hata wawili ama mmoja kuomba mkopo .

Alisema serikali ya wilaya haitapenda kuona vijana wakizurula mtaani ama kushinda Vijiweni bila kazi na kuwa watakaokamatwa watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili wafungwe gerezani wakafundishwe kufanya kazi huko.


Akielezea Kuhusu mafunzo hayo aliwataka vijana waliobahatika kuzingatia masomo hayo  na kutokukatishwa tamaa na changamoto wanazokumbana nazo bali wajipe moyo na kuamini kuwa wakati wao wa kuinuka ni sasa hivyo hawana budi kukabiliana na changamoto hizo.

Aidha aliwataka kutumia fursa hiyo ya mafunzo vizuri kwani serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasan imejipanga vyema kuwainua na kuwasaidia wahitaji wote kutokana na kutenga fedha nyingi katika Halmashauri zao hivyo wanachotakiwa kufanya ni kujitambua .

Aliongeza kuwa baada ya kupata mafunzo hayo jambo la msingi ni kuyatekeleza kwani utekelezaji wao utapunguza mazingira ya vitendo vya uhalifu na ukatili wa kijinsia katika jamii zao  huku akiwataka kuwatumia viongozi wao wakati wanapohitaji msaada

Wakizungumzia baada ya mafunzo hayo  wanufaika hao walisema wamejipanga vyema katika kuyapokea mafunzo kwani wanaamini ndoto zao za muda mrefu zitatimia lakini pia wataweza kumudu maisha yao pamoja na kuzikabili changamoto za maisha kwa ujumla.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Dkt. Heriel Mfangavo alisema mafunzo hayo yamejikita katika kuwasaidia vijana namna ya kujitegemea katika nyanja zote ili waweze kujikwamua katika changamoto wanazozipitia lakini pia kujiinua kiuchumi kwa kufanya shuguli mbalimbali za ujasiriamali 

Dkt Mfangavo aliongeza kuwa vijana ambao wanastahili kukaa kwenye makundi baada ya  mafunzo hayo wananufaika kwa kupata mikopo kutoka katika bajeti za halmashauri ambayo itawasaidia katika kuendeleza biashara zao lakini pia vijana ambao ni walemavu wanapewa kipaumbele cha kuweza kukopeshwa au kuingizwa kwenye fursa za ajira rasmi .

Meneja wa mradi wa YAM Zilpa Mgeni alisema   mradi huo unaendeshwa Kwa ushirikiano  na serikali na hivyo wanaishukuru  serikali kwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na mradi wao ambao kiujumla una msaada mkubwa sana kwa vijana 

''Mimi na timu yangu tumeona huu mradi unasaidia kwasababu tumegundua kuwa kuna mbadaliko makubwa tangu tumeanza kuwabainikwani hapo mwanzo walikuwa hawajiaamini kwamba wanaweza kufanya biasharalakini baada ya kupata mafunzo ya saikolojia na ujasiriamali wao wenyewe wamekiri  kwamba wanaweza kufanya kitu ''. alisema  Zilpa

Pia aliiomba serikali kuzidi kutoa ushirikiano hasa kwa kusaidia kupatikana kwa mikopo hiyo ili wanufaika hao wapate mitaji na kuweza kujiendeleza kimaendeleo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na diwani wa kata ya Luhunga Festo  Mgina aliwataka vijana hao  kusikiliza vyema mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwa pamoja na kuwahakikishia kupata mikopo baada ya mafunzo  yao kutokana na serikali kujipanga vyema katika kuwasaidia wahitaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI