Adeladius Makwega-DODOMA
Warufiji ni kabila lenye makundi makubwa matatu kwanza wale wanaoishi jirani na Mto Rufiji wanaozungumza KIRUFIJI hawa huwa wanazungumza taratibu, Wapo wale wanaoishi jirani na bahari wanazungumza KINYAGATWA na wapo wale wanaoishi milimani gongoni hawa wanazungumza KINDENGEREKO hawa wanazungumza kwa haraka haraka.
Ndiyo kusema WARUFIJI, WANYAGATWA na WANDENGEREKO wote hao kwa pamoja ni wa WARUFIJI tu kinachowatenganisha ni wapi wanapotokea katika eneo hilo jirani na Mto Rufiji.
Kabila hili linapatikana katika wilaya ya Rufiji nchini Tanzania ambapo kwa upande wa Kaskazini wakipakana na Wazaramo, Magharibi wakipakana na Waluguru na kwa upande wa kusini wakipakana na Wamatumbi, Wamwera na Wangindo.
Sehemu kubwa ya watu wa kabila hili wanatokana na makabila ya Wamatumbi, Wahehe na Wanyagatwa (hawa ni sehemu ya kabila hilo)
Katika Kabila hili wapo wale wanaoishi kandokanao ya Mto Rufiti hawa ni Warufiji wa asili ambapo kwa asili wanafahamika kama ALWII. Alwii maana yake watu wanaoishi jirani na maji. Pia wapo wale wanaoishi katika vilima Kirufiji wanaitwa MAGONGO kirufiji jina hilo maana yake kilima. Pia wapo wale wanaoishi kando ya bahari ambao wanafahamika kama WAVISIWA kama nilivyowagawa hapo juu.
Neno utani kwa Kirufiji ni Ung’ongo kulingana nao utani una maana ya hali ya kutokuwa sawa baina ya mtu mmoja na mwingine
Kwa kabila hili utani huwa unamaanisha udugu lakini si udugu wa damu. Hawa Wamatumbi, Wahehe na Wanyagatwa pengine hata Wangoni ambao walifika katika eneo hilo katika makundi ya watu wachache wachache walianza kuishi wakikaa kama LUKOLO (koo).
Wangoni wlaiotawanyika baada ya vita waliingia katika ukanda huu na kuchanganyika na Wahehe, Wamatumbi na Wanyagatwa hapo ndipo wakatokea Warufiji kuoleana.
Kuoleana huko koo hizo kadhaa ziligawanyika katika makundi makubwa kadhaa ya asili nayo ni wale wa Kusini Magharibi Wahehe na wale wa Kusini ambao ni Wamatumbi.Koo hizo ni MCHUCHULI, MKETO na MOMBOKA.
Kwanza kabisa ukoo wa MCHUCHULI-asili yao ni Wamatumbi hawa wanatoka Kusini na Watani wao ni ukoo wa MKETO. Pili ni ukoo wa MKETO hawa asili yao Uheheni wanatokea Kusini Magharibi na Watani wao ni ukoo wa MCHUCHULI.
Tatu ni Ukoo wa MOMBOKA asili yao ni Wamatumbi wanatokea Kusini na Watani wao ni ukoo wa MKETO. Hapo kuna koo nyingine kadhaa ambazo zinaangukia katika koo hizo kubwa tatu yaani MCHUCHULI, MKETO na MOMBOKA.
Akina MCHCHULI wanakoo zingine kama Ngayonga, Kweli, Lisukila, Nganga, Liganga, Libuye, Kilambo, Mkinua na Mlawa. Ukoo wa MKETO wana koo zingine kama Ungendo, Ngwengo, Mpili, Mkangama, Nwambo, Jimka, Sule, Mkumba, na Malinda. Ukoo wa MOMBOKA wana koo zingine kama Matimbwa, Ngwelle,Makando, Mkamba, Mtumbuka, . Mwopei na Msombokalso
Je kipi kitaendelea subiri matini ijayo.
Nakutakiasiku njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
0 Comments