Header Ads Widget

WAZIRI MKUU ATEMBELEA UJENZI WA SOKO LA MACHINGA COMPLEX

 


Na Hamida Ramadhan Dodoma 


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea ujenzi wa soko la  machinga Complex lililopo katika eneo la Uwanja wa ndege huku akiwataka wakurugezi ,wakuu wa wilaya ,na wakuu wa mikoa mingine kuiga mfano wa mkoa wa jiji la Dodoma lilivyotumia mapato yake ya ndani  kujenga soko hilo .


Hayo ameyasema leo jijini hapa wakati alipofanya ziara fupi ya kuona Maendeleo ya ujenzi Machinga Compex ambapo amesema ujenzi wa eneo hilo ni mkombuzi kwa wamachinga wote wa jiji la Dodoma. 


Amesema  ujenzi huo wa eneo la biashara litakuwa ni eneo la utalii ambapo wakuu wa mikoa kutoka mikoa 12 watakuja kujifunza katika soko hilo bora kuliko majengo yote yaliopo hapa nchini .


Aidha amewataka wakuu wa Wilaya na wakurugenzi kwenda kuwauganisha pamoja wafanyabiashara wote ili iwe rahisi kupatiwa mitaji na kuweza kusaidiwa katika shida nyingine.


" Wakuu wa wilaya anzeni kuwaweka pamoja wafanyabishara wote nchini na wenye bidhaa zinazofanana ili iwe rahisi kwao kupata mikopo na kuendekeza biashara zao," amesema Majaliwa.


Awali akisoma taarifa ya ujenzi huo Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema jiji la Dodoma linafanya juhudi kuhakikisha eneo hilo linakamilika kwa wakati ambapo kwa ujenzi wa awali watachukuliwa wajasiriamali 2000 kuweza kufanya biashara katika eneo hilo.


Pia amesema kukamilika kwa soko hilo jiji la Dodoma litaweza kukusanya Shilingi Bilion 1 kwa mwaka kutokana na tozo mbalimbali zotakazotozwa katika katika eneo hilo. 


Kwa upande wake Waziri kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Innocent Bashungwa amelipongeza jiji la Dodoma kwa kuwa wabunifu kwa kuweza kutengeneza soko hilo la wazi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo Maarufu kama machinga .


" Wakuu wa mikoa mingine igeni mfano huu mzuru wa mkoa wa Dodoma  katika ujenzi huu kueni wabunifu kulingana na maeneo lenu au mikoa yenu mnayofanyia kazi," amesema Bashungwa


Naye Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Joyce  Ndalichako amesema machinga wa mkoa wa Dodoma hawatakuwa na shida tena kwani sasa wanaweza kufanya kazi katika mazingira mazuri licha ya hapo awali jambo hilo kuonekana kama ndoto.


" Vijana kumbekeni Rais wa awamu ya sita onaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewajali wajasiriamali  hivyo niwaombe vijana msichague kazi kwani eneo hilo limejengwa kwaajili ya machinga tuchangamkie fursa katika eneo hili," amesema Waziri Ndalichako.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI