Header Ads Widget

WANAWAKE WATAKIWA KUWASAMEHE WAUME ZAO PINDI WANAPOWAKOSEA




WANAWAKE katika Wilaya ya Muleba mkoani Kagera wametakiwa kuwasamehe waume zao pindi wanapowakosea, ili kupunguza migogoro katika familia ambayo inasababisha kuwepo kwa mauaji na vitendo vya watu kujinyonga hasa wanaume.


Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambayo katika wilaya hiyo yamefanyika katika kata ya Rulanda, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Toba Nguvila, amesema kuwa haiwezekani wilaya yake ikawa ni mahala pa kuzika watu wanaopigana kwa vitu vizito na kujinyonga.


"Hivi sasa tunavyoongea hapa, nimepata taarifa leo hii huko Kamachumu kuna mwalimu amejinyonga, tufikie mahala Muleba iwe sehemu yenye amani, upendo, mshikamano na pia iwe sehemu ya kujadili masuala ya maendeleo tu, badala ya watu kupoteza muda kushiriki misiba ya waliouawa au kujinyonga, muda huo utumike kuzalisha mali" amesema.



Kwa upande wake msaidizi wa kisheria kutoka Ofisi ya Umoja wa Wasaidizi wa Kisheria wilayani Muleba, Aidath Buhile amesema kuwa katika kipindi cha mwaka jana walipokea migogoro 538 ya ukatili wa kijinsia.


"Lakini pia tulipokea migogoro 162 inayohusiana na matunzo ya watoto, akina baba wametelekeza watoto, na hilo linafahamika sasa akina mama wengi wanabeba mzigo wa kulea watoto peke yao" amesema Aidath.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI