Header Ads Widget

WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA FEDHA ZINAZOSADIKIKA ZA WIZI KIASI CHA ZAIDI YA TSH BILIONI 2.1

 




JESHI la  polisi mkoa  wa Iringa linamshilia  watuhumiwa  10 akiwemo wakala  wa  kampuni ya  Selcom Paytech Limited  kijana Tyason Kasisi  ambaye  alikuwa  akitoa  huduma ya  Selcom Pay  kwa  wizi  wa  fedha   kiasi cha  zaidi ya shilingi bilioni  2,129,856,000 mali ya kampuni ya Selcom Paytech Limited .


Kamanda  wa  polisi wa  mkoa wa Iringa Allan Bukumbi  aliwaeleza   waandishi wa habari  kuwa   mtuhumiwa huyo  kupitia   huduma ya Selcom pay   isiyo haliali  alihamisha  fedha  kwenda  kwenye namba mbali mbali  za simu  na  kisha  kuchukuliwa taslimu kupitia  wakala wa  huduma  za  kifedha  za mtandao mbali mbali ya  simu pamoja na akaunti  za Benk.


“ wizi  wa fedha   hizo  ulifanyika  kwa njia ya  mtandao katika  mkoa wa Iringa ,Dar es Salaam  na Morogoro  kati ya tarehe 9 hadi tarehe 27 Novemba 2021 baada ya wakala huyo Tyason Kasisi  kufanikiwa kuchezea mfumo wa  kieletroniki  wa  “Selcom Pay’ unaomilikiwa  na kampuni ya  Selcom Paytech Limited” alisema kamanda  Bukumbi

Kuwa  wakala  huyo  kwa njia ya udanganyifu  alianza kujitumia  fedha   pamoja na  kuwatumia  watu wengine  na  kwa kushirikiana  na  genge  la uhalifu  walifanikiwa  kuiba kiasi  hicho  cha Tsh 2,129,856,000

Hata   hivyo  alisema  jeshi la  polisi  limefanikiwa  kukamata  (kuokota)  fedha  kiasi cha shilingi 956,974,000 kutoka  kwa  watuhumiwa  na  washirika wa uhalifu  huo  ambao walipokea  sehemu ya fedha   hizo   kwa njia ya  kuzificha katika  maeneo  mbali mbali  ikiwemo  makazi  na shambani  pia   kiasi cha fedha  shilingi  121,215,783 zimezuiliwa katika  moja ya benk za  kibiashara  mkoa wa  Iringa ikiwa ni mali ya  uhalifu .

Alisema  kuwa  upelelezi  uliofanywa hadi sasa   umebaini  kuwa  genge  hilo la uhalifu na wizi wa fedha  za kampuni  hiyo  uliongozwa na  watu  watatu  ambao ni Tyson Kasisi ,Patrick Chalamila na  Evaristo Chalamila ambao  wamebaikika kuwa ni wanufaika wakuu  wa uhalifu  huo .

 Aidha  alisema  mbali ya  fedha  hizo kukamatwa pia  mali  zinazosadikika kuwa za  uhalifu  huo  zimekamatwa  na kuhifadhiwa  ikiwa ni pamoja na magari manne  yenye thamani ya Tsh 303,000,000 .

                            Kamanda  Bukumbi  alitaja  mali  hizo kuwa ni  Scania yenye  jina la  mtuhumiwa Patrick Chalamila  lenye thamani ya  shilingi  milioni 128, Mitsubish Fuso yenye usajili namba T 796 DXV yenye jina la mtuhumiwa  Tyson Kasisi  likiwa ni thamani ya shilingi  milioni 75, gari aina ya  Toyota Harrier lenye usajili T 719 DXX lenye  jina la Tyson Kasisi  likiwa na thamani ya  shilingi milioni 72 na gari aina ya  Nissan Juke lenye usajili T 605 DXV lenye jina la Patrick Chalamila likiwa na thamani ya  shilingi milioni 28.

 Pia  jeshi la  polisi  limekamata gari aina ya  Toyota  IST  yenye  namba za usajili  T 576 DRN mali ya Patrick Chalamila lililotumika kufanikishia uhalifu  kwa  kusafirisha fedha  hizo za wizi  kutoka Madibila  wilayani Mbarali  ,Ilula wilaya ya  Kilolo  kwenda kuzificha Kilombero  mkoani Morogoro.

 Kamanda huyo  alisema  kuwa ushahidi uliokusanywa  hadi sasa  umetosha kuwafikisha   watuhumiwa 10  mhakamanani  kujibu  tuhuma  zinazowakabili za  kuongoza genge la uhalifu pamoja na kujipajia  fedha kwa  njia ya udanganyifu .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI