Header Ads Widget

SHULE 2 ZA "HIGH SCHOOLS"MASOMO YA SAYANSI KUANZA JULAI MOSI MUSOMA VIJIJINI

 

Na Shomari Binda Matukio Daima Media -Musoma 

MUSOMA Vijijini inatarajia kufungua shule 2 za kidato cha 5 na 6 zitakazofundisha masomo ya sayansi zitakazoanza rasmi julai mosi 2025 baada ya kukamilishwa taratibu zote za utoaji elimu.


Shule hizo ni Suguti High School itakayoanza na wanafunzi 158 pamoja na Mugango High School itakayoanza na wanafunzi

62 ambao tayari wamesha sajiliwa.

Taarifa iliyotolewa juni 8,2025 na ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo imesema mbunge wa jimbo hilo atazitembelea shule hizo na kuzungumza na wanafunzi hao.

Licha ya kuzungumza na wanafunzi atawagawia vitabu vya masomo ya sayansi ili kuanza muula wa masomo wakiwa hawana changamoto ya vitabu.

Baadhi ya wadau wa elimu waliopokea taarifa hiyo wakiwemo wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini wamemshukuru mbunge huyo kwa jitihada zake za kuinua elimu.

Wakizungumza na Matukio Daima wamesema mbunge huyo ni mfano wa kuigwa katika kufatilia na kuhimiza masuala ya elimu.

Juma Mhina mkazi wa Kata ya Mugango amesema juhudi za mbunge huyo kwenye elimu zinaonekana kuanzia elimu ya awali,msingi hadi sekondari.

Amesema wananchi wanapaswa kumuunga mkono kutokana na juhudi hizo kubwa anazozifanya kwenye sekta hiyo.

" Tumeona taarifa kutoka ofisi ya mbunge juu ya kuanza masomo ya kidato cha 5 na 6 kwa kweli tunamshukuru kwa jitihada hizo.

" Kwa hili hatupepesi macho tunamuomba agombee tena kwenye uchaguzi wa 2025 na tunaahidi kumchagua ili aendelee kutuletea maendeleo yakiwemo ya elimu kwa watoto wetu",amesema.

Sekondari nyingine zinazokaribia kukidhi vigezo vya uwepo wa High Schools za sayansi ni Mtiro Secondari iliyopo  Kata ya Bukumi,Makojo Sekondari, Kata ya Makojo iliyopo Kata ya Bugwema Sekondari, Kata ya Bugwema,Kiriba Sekondari, Kata ya Kiriba 

 Nyakatende Sekondari, Kata ya Nyakatende na Etaro Sekondari iliyopo Kata ya Etaro 

Vigezo muhimu kwa shule hizo ni pamoja na kuwa na maabara 3 za masomo ya sayansi,Bweni,Bwalo la chakula,Maji ya bomba pamoja na Umeme

Sekondari mpya zote zilizopata uwekezaji mkubwa kutoka serikalini kwenye jimbo la Musoma Vijijini zina maabara tatu za masomo ya sayansi ambazo ni Kabegi (Kata ya Ifulifu), Kurwaki (Kata ya Mugango), Wanyere (Kata ya Suguti), Kasoma (Kata ya Nyamrandirira), na Butata (Kata ya Bukima)



Mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo ameendelee kuwaomba wananchi kuchangia kuongeza High Schools za Masomo ya Sayansi jimboni humo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI