Header Ads Widget

LHRC WATAKA MCHAKATO WA MABORESHO YA SHERIA ZA HABARI KUSHIRIKISHA WADAU

 



Kituo Cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC) kimeiomba Serikali kwa kushirikiana na wadau wa habari kutoa maoni ya kina yatakayochangia kuboreshwa kwa sheria za habari..,............Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam.



Pia, kuhakikisha mchakato wa maboresho ya sheria unashirikisha wadau wengi pamoja na kufanya mapitio ya sheria zote zinazogusa Sekta ya habari na upatikanaji wa taarifa nchini.


Wito huo ameutoa leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, alipokua akitoa pongezi kwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kufungua mlango wa majadiliano ya kuboresha sheria ya Habari.


Amesema kuwa, licha ya magazeti hayo kushindwa kesi lakini bado hayajapatiwa leseni, hivyo tamko la Waziri Nape kuyafungulia magazeti hayo imekua ni kiashiria kizuri cha kurudi kwa uhuru wa vyombo vya habari, hivyo ni muda muafaka sasa wa kuangalia changamoto za kiujumla za sheria inayoikabiki Sekta ya habari na uhuru wa kujieleza. 


Aidha, amesema kuwa, sheria za habari zilizopo kwa sasa bado zinaendelea kuumiza haki ya kupata taarifa kama ilivyoainishwa katika ibabara ya 18 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambapo athari yake imeathiri magazeti, Radio, Television,mitandao ya kijamii na uhuru wa internet.


Hata hivyo, amesema LHRC imekua ni mdau mkubwa wa habari sheria za habari ambapo imekua ikifanya uchechemuzi kwa muda mrefu tangu kuibuka kwa wimbi la utungaji wa sheria zinazoweka ugumu kwa vyombo vya habari kufanya kazi zake, piah kwa kiwango kikubwa sheria hizo zimekwamisha urahisi wa upatikanaji wa taarifa kwa jamii.


"Tumeshuhudia kurejeshwa kwa lessen za magazeti manne ikiwemo gazeti la Mwanahalisi lenye namba 0000433, Mawio lenye leseni namba 0000437, Mseto lenye leseni namba 0000436 na Tanzania Daima lenye leseni namba 0000434,  kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan"amesema Henga.


Aidha, amesema miongoni mwa sheria zinzzokwamishwa kuwepo kwa uhuru wa habari ni pamoja na sheria ya makosa ya mtandao,  ya mwaka 2015 , Sheria ya upatikanaji wa habari ya mwaka 2016, sheria ya mamlaka ya mawasiliano pamoja na kanuni zake, na sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016. 


Hata hivyo, amesema wanaimani na Serikali kwamba itaendelea jitihada za kukuza na kuendeleza na uhuru wa vyombo vya habari maslahi na ulinzi wa waandishi wa habari pamoja na kudhibiti ufungiaji holela wa vyombo vya habari, pamoja na kuweka mazingira rafiki Ili kurejesha hali ya uchumi wa vyombo vya habari vilivyoathirika na sheria hizo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI