WAZIRA ya Maji kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA), umesaini mikataba 86 ya ujenzi wa miundombinu ya Maji yenye thamani ya Sh.Bilioni 309.99.Mwandishi Hamida Ramadhan MDTV Dodoma
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika hafla ya Utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji vijijini ambapo amewataka wakandarasi kufanya kazi pasipo ubabaishaji pamoja na kutekeleza miradi hiyo kwa kuzingatia taaluma na weledi ili kuwa na miradi yenye ubora na endelevu.
"Niwatake wakandarasi muende mkafanye kazi kwa weled msilete ubabaishaji miradi yenye ubara na endelevu izidi kuwepo," amesema Waziri Aweso .
Kwa upande wake Mkurungezi Mtendaji wa RUWASA, Mhandisi Clement Kivegalo amesema kuwa RUWASA imepanga kutekeleza miradi 1,527 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 351 ilikuwa ya utafutaji wa vyanzo vya maji na usanifu wakati miradi 1,176 ni miradi ya ujenzi wa miundombinu.
Kwa upande wao wakandarasi waliopewa tenda za miradi hiyo amesema kuwa watafanya kazi kwa weledi ,uaminifu na ushirikiano ili kuhakikisha jamii iishio vijijini inapataa huduma ya maji safi na salama.
Dhamiran ya Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) ni kutoa na kusimsmiahuduman ya maji safi na salama na kuhamasisha usafi wa mazingira kwa jamii iishio vijijin kwa ushirikiano,weledi na kwa gharama nafuu.
0 Comments