Header Ads Widget

DARAJA LA JPM KIGONGO- BUSISI KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI KANDA YA ZIWA.

NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA.

 MWANZA.Katika kuelekea kuadhimisha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Ujenzi imeeleza mafanikio yake makubwa likiwemo kukamilika kwa ujenzi wa Daraja la JPM linalounganisha Kigongo na Busisi mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa kuondoa kero ya kusubiri kivuko kwa zaidi ya masaa mawili hadi matatu.

“Daraja hili ni mkombozi kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa. Awali walikuwa wakipoteza muda mwingi kusubiri kivuko. Kwa sasa, muda huo utapungua kwa kiasi kikubwa na shughuli za kiuchumi zitachangamka zaidi,” alisema Waziri Ulega.

Ulega alifafanua kuwa mradi huo mkubwa umegharimu takribani shilingi bilioni 716 na umejengwa kwa viwango vya kimataifa, ukiwa ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayoendeshwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Mwanza wameishukuru serikali kwa hatua hiyo ya kihistoria na kuiomba iharakishe ufunguzi rasmi wa daraja hilo ili magari yaanze kupita na kuondoa usumbufu uliopo kwa sasa.

“Tunampongeza Rais Samia kwa kazi hii kubwa. Tumekuwa tukiteseka kwa foleni ndefu za kivuko. Tunaomba sasa daraja lifunguliwe mapema ili tuanze kulitumia,” alisema mkazi hao wa Busisi.

Daraja hilo la JPM linatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Juni 2025, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka minne ya uongozi wake.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI