Header Ads Widget

SERIKALI KUKUZA TASNIA YA FILAMU

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imedhamiria kukuza Tasnia ya Filamu nchini Tanzania ili kutangaza fursa zilizopo ili kuwawezesha Wadau wa Tasnia kufaidika zaidi na kazi zao.Mwandishi Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Kauli hiyo, ameitoa jijini  Dar es salaam alipokutana na Waandishi wa Habari  alipokuwa akiagana na Wasanii wa Tamthilia ya Huba inayorushwa na kituo cha DSTV  waliokuwa wakielekea Jijini Dubai katika Falme za kiarabu (UAE) baada ya kualikwa  kwenda kutekeleza majukumu yao ya kikazi.


Amesema kuwa, kwa sasa ni muda muafaka kwa Serikali kuwashika mkono  wasanii kwani kwa muda mrefu wamekua wakijafanya juhudi wao wenyewe ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kukuza tasnia hiyo.



Aidha, amesema  kuwa Serikali ina dhamiria kuinua na kuendeleza Tasnia ya Filamu nchini kwa kuwa Filamu zao ni chachu ya kutangaza lugha ya Kiswahili pamoja na Tamaduni zetu.


Hata hivyo, amesema ukuaji wa Sekta ya Filamu nchini umeendelea kuonesha taswira chanya na hasa tukiangalia tulipotoka na hapa tulipo.


"Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan tayari imetenga fedha za maendeleo ya Sanaa na Michezo kiasi cha Shillingi Billioni 2.5 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni," amesema Mchengerwa.



Kwa upande wake, Mtayarishaji na Muongozaji wa Tamthilia hiyo, Azizi Ahmed ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wa kuendeleza na kuiinua Tasnia ya Filamu na kuahidi kuendelea kuitangaza Tanzania ndani na nje ya Nchi kupitia Tamthilia yao.


Awali  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Elia Mjata  aliwapongeza Watayarishaji wa Tamthilia hiyo, na kutoa rai kwa Wadau wengine kuongeza ubunifu katika utendaji wao ili kutayarisha kazi zenye ubora.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI