MJUMBE wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (NEC) Salim Asas amechangia kiasi cha shilingi milioni 5 kuwezesha kukufuliwa kwa mfuko wa kusaidiana wakati wa shida kwa wanachama wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) tawi la chuo kikuu cha Iringa .
Akizungumza baada ya kuchangia fedha hizo jana kupitia mnada wa keki iliyoandaliwa na wanachama hao chuoni hapo Asas alisema kuwa suala la wanachama wa tawi hilo la chuo kikuu cha Iringa kuwa na mfuko wao wa kusaidiana ni jambo la msingi na litasaidia kupunguza changamoto za wanachama pindi wanapokwama .
Kuwa kupitia mfuko huo wa kusaidiana utakaoanzishwa ni hatua moja wapo ya wanachama kuondokana na kero ya kutafuta njia ya kumsaidia mwanachama mwenzao pindi anapopatwa na shida .
“ Pamoja na kufikiria kuanzisha mradi wa tawi ila hili la kuanzisha mfuko wa kusaidiana kwenu ninyi ni ukombozi mkubwa maana wakati mwingine unakuta mwanafunzi mwenzenu anakabiliwa na changamoto ya laki moja ili kutatua changamoto yake pindi anaposubiri mambo yake ya kifedha kuwa vizuri inakuwa rahisi kukopeshana kupitia mfuko huu” alisema
Pia alitaka suala la kuanzisha ujenzi wa ofisi ya UVCCM tawi la chuo kikuu cha Iringa kufanyiwa kazi haraka ili kuweza kuwa na ofisi itakayofanya shughuli za chama .
MNEC Asas alisaema kwa upande wake amekuwa mdau mkubwa wa chuo hicho cha Iringa pamoja na kuhakikisha wanachama wanaendelea kutimiza majukumu yao ndani ya tawi hilo .
Hata hivyo alisema ili tawi hilo kuweza kufanikiwa zaidi ni lazima kuwa na malengo sahihi ya kukitumikia chama badala ya kutaka chama kiwatumikie kwani wapo baadhi ya watu wanajiunga na chama ili kutafuta nafasi za uongozi jambo ambalo si sawa .
Kuwa nafasi za uteuzi ndani ya chama na serikali ni nafasi ambazo zinakuja zenyewe na sio kuzitafuta kwa nguvu pale unapofanya vizuri kwenye chama ndipo mwanzo wa kuteuliwa na sio wewe kutafuta teuzi .
Aidha aliwataka wanachama wa CCM kila mmoja kwa nafasi yake kuendelea kueleza mambo mazuri na makubwa ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiyafanya katika taifa hilo kwa kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo .
Awali wakizungumza katika hafla hiyo makada wa CCM Itiwen Samson na Richard Kasesela walisema kuwa mchango wa MNEC Asas katika maendeleo ya Iringa ni mkubwa sana na kuwa ni vigumu kuyaelezea .
Kasesela alisema kuwa pamoja na Asas kusaidia chama ila amekuwa msaada mkubwa wa kuchangia maendeleo ya mkoa wa Iringa katika afya ,elimu na hata mtu mmoja mmoja wakiwemo wanafunzi kuwasaidia kusoma.
0 Comments