Header Ads Widget

WAUZAJI WA VIFAA VYA UJENZI KIBAHA WALIA NA SERIKALI

 



BAADHI ya wauzaji wa vifaa vya ujenzi Wilayani Kibaha mkoani Pwani wameiomba serikali kuweka utaratibu wa wamiliki wa viwanda au mawakala wakubwa wa wauzaji wa vifaa vya ujenzi vinavyozalishwa kwenye mkoa huo kuwa na stoo za kuuzia vitu vinavyozalishwa badala ya stoo au maduka hayo kuwa Jijini Dar es Salaam ili kupunguza bei ya vifaa hivyo. 


Akizungumza na MatukioDaima Mjini Kibaha mfanyabiashara mdogo wa vifaa vya ujenzi Maili Moja Wilaya Kibaha Mohamed Mchicha alisema kuwa mkoa wa Pwani unaongoza kwa kuwa na viwanda lakini viwanda vyote havina stoo wala mawakala wakubwa hivyo bidhaa zikizalishwa zinapelekwa kwenye stoo au kwa mawakala wakubwa nao kwenda kununua na kuzirudisha Pwani.


Mchicha alisema kuwa vifaa vyote vikitengenezwa kuuzwa vinauziwa Dar es Salaam na wao wanakwenda kununua huko na kuzileta Pwani ili hali vifaa hivyo vinazalishiwa Pwani.


"Tunaiomba serikali kuliangalia hilo kwa kuweka utaratibu wa wenye viwanda kuwa na stoo za kuuzia bidhaa hapa au mawakala wakubwa nao kuwa na stoo hapa badala ya bidhaa zinapotoka kiwandani kwenda kuuziwa Dar es Salaam ambapo husababisha bei kuwa juu," alisema Mchicha.


Alisema kuwa vifaa hivyo vingekuwa vinauziwa hapa kidogo bei zingekuwa nafuu na wananchi wasingelalamika ambapo kwa sasa wanafikiri wao wanapandisha lakini wao wanauza kutokana na manunuzi waliyonunulia.


"Maana ya kuwa na viwanda ni kupata unafuu wa bidhaa lakini utaratibu uliopo kwa sasa siyo mzuri na si rafiki kwani haiwezekani bidhaa zizalishwe hapa lakini tukanunulie Dar es Salaam kwa nini zisiuziwe sehemu zinapozalishwa ili kuwapunguzia gharama wananchi," alisema Mchicha.


Aidha alisema hiyo ni changamoto inayowakumba katika kuwahudumia wananchi ambapo vifaa vya ujenzi kwa sasa vimepanda bei maradufu na kusababisha wateja kulalamika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI