Header Ads Widget

BARAZA LA WAISLAMU TANZANIA (BAKWATA )MKOA WA KILIMANJARO KUJENGA MSIKITI MKUU WA MKOA

 


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai amepongeza baraza kuu la kiislamu Bakwata mkoa wa Kilimanjaro kwa kuja na maono ya kuanzisha msiki Mkuu wa mkoa ambao utatoa fursa kwa waumini wa dini hiyo. 


Mkuu wa mkoa huyo ametoa pongezi hizo wakati akiwa katika sherehe za maulidi ya mkoa iliyofanyika katika viwanja vya ofisi za barabaza hilo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.


Aidha amesema kuwa pindi msikiti huo utakaojengwa utawakutanisha waislamu, na itawapa nafasi ya kujadili Mambo mbalimbali yanayohusu Imani kwa utulivu ,lakini kikubwa itawasaidia kuwajenga waumini kiimani na kuwajengea hofu ya mwenyenzi Mungu.



"kupitia hadhara hii naomba niwapongeze kwa kujitokeza kwa wingi na nitumie fursa hii kuwasa kuendelea kuwa na umoja na mshikamano , mkifanya  hivyo mtakuwa mnafanya vyema Kama maneno ya mwenyenzi Mungu yanavyotuasa kwenye kitabu Cha kuruani tukufu ,nimebahatika kuona Aya ya tatu sura ya kumi na tatu,imbayo imewaasa kushikamana kwa maana ya dini"Alisema Kagaigai.


Pia amewasa waumini wa dini hiyo ya kiislamu kushikamana kwa kuwa na umoja pomoja na kuwa na umoja kwa kuwa dini nyingine na viongozi wao kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya Taifa kwani kukiwa na umoja na mshikamano hakutakuwa na nafasi ya kuleta majungu na fitna kwa mtu mmoja mmoja .


Hata hivyo amewataka viongozi hao kuwa wawazi  katika kuwambia waumini wao mapato na matumizi yanayoingia ili kuepusha migogoro isitokee , kwani kwa kufanya hivyo hakutakuwa na majungu fitina Wala chiki ,na pia watakuwa na moyo wa kusaidia katika maswala ya maendeleo.


kwa upande wake Katibu wa Bakwata mkoa wa Kilimanjaro Awath Lema amesema kuwa wa Kuna baadhi ya waislamu Wanaleta vita ndani ya uislamu ambapo amesema kwa kipindi kirefu walikuwa wanatafuta mchawi ni nani kumbe uchawi upo ndani ya yawaislamu wenyewe.



Amesema kuwa waislamu wenyewe ndio wamekuwa mstari wa mbele kupambana na mafanikio ya waislamu kwa kupitia katika maeneo mbalimbali kupinga maendeleo yanayoletwa na baraza hilo.


Sisi tunasimamisha miradi mengi na tunajitahidi ,tuko nyuma sana na hatuwezi kujilinganisha na ndugu zetu wakristo ambao wapo mbali ,ukiangalia Mashule walizonazo ,mahosipitali walizonazo ,ukiangalia na vitega uchumi vingi walivyonavyo ,sisi hatuwezi kushindanda nao Sasa tunajiuliza ni wapi tunakwama ,wapi tunakosea na wapi tunashindwa ,lakini tunakuja kupata majibu ya kwamba sisi tunashindwa pale wenzetu wanavyotivuruga "Alisema Awath.

 

Hata hivyo makatibu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro wametoa tamko la kuwaonya baadhi ya waislamu wanaovuruga  mipango ya maendeleo inayopangwa na baraza hilo pamoja na kuwa makini na wote wasioitakia taasisi hiyo mafanikio.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI