Header Ads Widget

FUNZA WATUMIKA KUNENEPESHA KUKU WA KIENYEJI



 


KIJANA Rodney Mwasha mkazi wa Mkoani wilayani Kibaha Mkoani Pwani amegundua lishe kwa kuku ambapo anatumia funza kunenepesha kuku wa kienyeji anaofuga na kuwauza


Akizungumza na mwandishi wetu Mjini Kibaha alisema kuwa kutokana na kutumia funza anapunguza gharama za kununua lishe ya kuku kwani wadudu hao ni lishe tosha.


Mwasha alisema kuwa funza wamesaidia kuku kunenepa na kuwauza kwa bei nzuri ya shilingi 20,000 kwa kuku mmoja ambapo amepata wateja wengi.


"Nilifikia hatua ya kuwalisha kuku funza baada ya kuona kuku kila anapowaachia hutafuta mauchafu na kula hao wadudu ndipo alipogundua na kuanza kuwazalisha kisha kuwapa kuku wake,"alisema Mwasha.


Alisema kuwa gharama ya kuwanunulia vitamini sasa haipo ambapo kwa mwezi alikuwa akitumia gharama kubwa kununua lishe ili kuboresha afya ya kuku.


"Baada ya kufanya utafiti na kugundua kuwa funza ni lishe nzuri nilianza kuwazalisha funza kwa wingi na kuwapa kuku ambapo wanakuwa na afya nzuri na wananenepa," alisema Mwasha.


Aidha alisema kuwa funza hao anawazalisha kupitia mabaki ya vyakula, matunda na uchafu wa aina mbalimbali.


"Tangu nianze kuwalisha kuku wangu funza nimekuwa na wateja wengi kwani wamekuwa na afya na ni wakubwa wana nyama za kutosha," alisema Mwasha.


Aliongeza kuwa pia anatumia magamba ya kono kono na kuyasaga kisha kuchanganya na mapumba na kuwalisha kuku wake.


"Magamba ya konokono yakisagwa na kuchanganywa na pumba ni chakula kizuri sana kwa mifugo wakiwemo kuku ambapo mimi huwa nawalisha kuku wangu,"alisema Mwasha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI