NA HADIJA OMARY LINDI...
Serikali Mkoani Lindi kutoa viwanja kwa Mahakama ya Mkoa huo kwa ajili ya ujenzi wa Majengo ya Mahakama za Mwanzo katika ngazi ya msingi kila kata ndani ya Mkoa huo
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Zainab Telack wakati wa uzinduzi wa wiki ya Sheria Nchini uliofanyika kikanda kwa njia ya kimtandao ZOOM MEETING ukumbi mdogo wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo
Ndemanga alisema ukosefu wa maeneo ya ujenzi wa majengo ya Mahakama katika ngazi ya kata ni miongoni mwa changamoto inayofanya kata nyingi katika mkoa huo kukosa mahakama za mwanzo
ambapo alieleza kuwa hatua ya Serikali ya Mkoa huo kutoa viwanja kwa mahakama kila kata kwa ajili ya kujenga mahakama za mwanzo itakuwa suruhisho tosha.
"Tumegundua changamoto ya kwanza ni upatikanaji wa maeneo mahakama za mwanzo zipo katika ngazi za Msingi kule kwenye kata lakini kata nyingi hazina viwanja kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama kwa hivyo hata pale mahakama inapokuwa na pesa inashindwa kujenga mahakama za mwanzo kutokana na changamoto hiyo ya maeneo" alisema Ndemanga.
Alisema katika Mpango huo kila kata inatapata kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa mahakama hizo za mwanzo kwani kwa kufanya hivyo kwa kiasi kikubwa tutapunguza upungufu wa Mahakama za Mwanzo katika ngazi za Msingi.
Kwa upande wake Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahaka ya hakimu mkazi Mkoa wa Lindi Consolatha Singano . alisema pamoja na kwamba uwepo wa mahakama za mwanzo kwa ngazi ya msingi kila kata ni takwa la kisheria lakini wananchi wa maeneo mengi ndani ya mkoa huo wa lindi wamekuwa wakilikosa ambapo inawalazimu kusafiri maeneo jirani ili kupata huduma hiyo ya mahakama
"Endapo Mkoa utatoa viwanja hivyo na Mahakama kujenga Mahakama za mwanzo ni wazi kwamba wananchi watasogezewa karibu huduma za kimahakama na itakuwa rahisi kuzifikia kwa haraka,Kwani huduma za mahakama zikisogea karibu na wananchi haki itapatikana kwa wakati na bila gharama"
0 Comments