Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Chama Cha ACT Wazalendo kinatarajia kufanya mkutana Mkuu maalum January 29, mwaka huu ambao umelenga kujadili muelekeo wa chama hicho kuelekea mwaka 2025.
Aidha, mgeni rasmi katika Mkutano huo anategemewa kuwa Rais wa chama kikuu cha upinzani kutoka nchini Zimbabwe Nelson Chamisa ambapo atatoa salam kwa watanzia na Dunia kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ado Shaib amesema kuwa, Mkutano huo utatanguliwa na mikutano mingine miwili ambayo itafanyika January 27 na 28 katika ukumbi wa Mlimani City.
Amesema kuwa, lengo la huo ni kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa pamoja na Makamo Mwenyekiti kutokana na majina yatakayopitishwa na Halmashauri kuu ya chama hicho.
Aidha amesema kuwa, January 28, kutakuwa na mdahalo wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa chama hicho, huku ikiwa January 29 kinatarajia kufanya mkutano Mkuu maalum,ambao umelenga kujadili muelekeo wa chama hicho kuelekea 2025.
Amesema kuwa, January 28, kutakuwa na mdahalo wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti kuanzia saa 10 jioni, na January 29 kutakua na Mkutano maluum kuanzia 3 asubuhi ambapo viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watahudhuria .
Ameongeza kuwa, siku hiyo hiyo ambayo kutafanyika Mkutano huo ifikapo saa moja jioni kutakua na uzinduzi wa App ya ACT kiganjani ambapo wananchi wataweza kupata taarifa na kutoa maoni na changamoto zao kwa njia rahisi.
Hata hivyo, amesema mbali na wajumbe wa Mkutano Mkuu na viongozi kutoka majimbo na mikoa na kamati kuu wa kuchaguliwa na kuteuliwa watashirikia viongozi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo kenya.
Aidha, amesema kuwa, katika mkutano huo utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa vya upinzani kutoka nchi ya Kenya, Zimbambwe, Zambai pamoja na Uganda,
Mbali na viongozi hao pia utahudhuriwa na wajumbe wa Mkutano viongozi kutoka majimbo na mikoa, kamati kuu wa kuchaguliwa na kuteuliwa huku akieleza kuwa tukio hilo ni muhimu sana na la kihistoria.
"Miongoni mwa vyama vitakavyoshiriki ni chama Kikuu cha upinzani Cha NDC Alliance kutoka Zimbabwe, chama Kikuu cha upinzani ODM kutoka Kenya, NUP kutoka Uganda, chama cha UPND kutoka Zambia, UTM kutoka Malawi pamoja na UNC Kongo"amesema Ado.
Mbali na vyama hivuo, pia watahudhuria viongozi mbalimbali kutoka Asasi za kiraia, wanazuoni, wasanii pamoja na vyama vya siasa kutoka nchini Tanzania.
0 Comments