Header Ads Widget

United v City: Ole kuendeleza ubabe leo dhidi ya Pep?


United v City: Ole kuendeleza ubabe leo dhidi ya Pep?

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Dabi ya Manchester ya 186 inapigwa leo Jumamosi katika dimba la Old Trafford, ni mechi kubwa katika ligi kuu England, ngumu na yenye ubabe, lakini ni wekundi wa Old Trafford au Wananchi wa Etihad watakaoibuka wababe leo?

"Najua Manchester City wamekuwa na matokeo yasiyoridhisha wakikutana na Manchester katika misimu ya hivi karibuni, lakini kuelekea mchezo huu, City wanapigiwa chapuo kushinda," alisema mchambuzi wa soka wa BBC Mark Lawrenson.

Katika utabiri wake Lawrenson anaipa ushindi City wa ugenini wa 1-2

'Ilikuwa Cristiano Ronaldo, Edinson Cavani na Bruno Fernandes, walioipa ushindi wa 3-0 dhidi ya Tottenham wiki iliyopita na wakafanya hivyo kwenye ligi ya mabingwa dhidi ya Atlanta, lakini waliruhusu magoli kirahisi dhidi ya Waitaliano hao, sioni kwa namna gani watawazuia City kufunga', alisema Mark Lawrenson.

Rekodi ya Ole dhidi ya Pep

Ole Gunnar Solsjaer amekuwa na rekodi nzuri za ushindi dhidi ya Pep tangu achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo. Amemchapa Pep mara nne na kuwa Kocha aliyemchapa Pep mara nyingi zaidi pale England.

Kitakachomsumbua Pep kingine ni soka la kushambulia kwa kushtukiza mtindo ambao United wamekuwa wakiutumia kama silaha hasa wanapokutana na timu ya aina ya City.

Huenda aina hii ya mchezo leo ikamsaidia Ole tena kuendeleza rekodi ya kumfunga Pep kwa sababu Pep na kikosi chake cha City hupata shinda ya kukabiliana na mashambulizi ya ghafla.

Tazama walichofanywa na Patrick Viera na kikosi chake cha Crystal Palace Juma lililopita, tena katika uwanja wa nyumbani wa City pale Etihad.

Ole ameiongoza United kutofungwa na City katika michezo minne mfulululizo, ikishinda minne na kwenda sare mmoja, ikiwa ni matokeo mazuri kwenye mechi nyingi zaidi tangu wacheze mechi sita dhidi yao bila kufungwa kati ya mwaka 2008 na 2011. Hii ni rekodi nzuri dhidi ya Pep katika mechi takribani 5.

Antonio Conte aliyejiunga na Spurs wiki hii, amekutana na Pep mara 4 wakati huo Conte akiifundisha Chelsea na kushinda michezo miwili, Luis Enrique akiwa kocha wa Barcelona amekutana na Pep mara 4 na kumfunga mara 2 huku Jurgen Klopp wa Liverpool amekutana na Pep mara 22 na kumfunga mara 9 tu. Hii inakuonesha Pep si kocha rahisi kufungika. Je rekodi ya Ole dhidi ya Pep kumbeba?

Mifumo, mtindo ama Mchezaji mmoja mmoja kuamua matokeo ama mfumo?

United imekuwa na wakati usio mzuri katika mechi zake za hivi karibuni. Baada ya kuchapwa kwa aibu hivi karibuni na Liverpool 5-0, wakamchapa Surs 3-0 kabla ya kwenda sare ya 2-2 na Atlanta katika ligi ya mabingwa Ulaya, Cristiano Ronaldo akionesha kwa nini ni mchezaji wa kuogopwa.

Leo United wako nyumbani, lakini hawana rekodi nzuri wakicheza nyumbani hasa mwaka huu, wakiruhusu kufungwa michezo 7 katika mashindano yote waliyocheza katika dimba lao la Old Trafford, ikiwa ni michezo mingi kupoteza nyumbani tangu itokee hivyo miaka 10 iliyopita mwaka 2001. Kwa hivyo rekodi hiyo itazidi kuongeza presha kwa Ole.

Pengine mechi ya leo, itaamuliwa na uwezo wa chezaji mmoja mmoja hasa kwa upande wa United. Mara nyingi huoni ikicheza kama timu kwa muda mrefu ikikutana na wapinzani wanaocheza kitimu.

Wakati kama huo Ronaldo, Edinson Cavani kwa uwezo wao na uezoefu wanapaswa kukaza buti.

United imekuwa na wakati usio mzuri katika mechi zake za hivi karibuni

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mfumo wa 3-5-2 waliotumia Man United katika mechi zilizopita hasa ngumu dhidi ya Spurs (Oktoba 2021) na kushinda 3-0, dhidi ya City (Machi 2020) na kushinda 2-0 na dhidi ya Chelsea (Februari 2020) na kushinda 2-0, uliwapa nguvu United na kuruhusu mashuti machache langoni mwake.

Huenda Ole akautumia mfumo huu uliompa matokeo mazuri hivi karibuni dhidi ya timu kubwa, ikianza na mabeki watatu na washambuliaji wawili ambao wanatarijiwa kuwa Cavan na Ronaldo.

Ukiacha mchezo huu na ule wa jana ambapo Southampton ilishinda 1-0 dhidi ya Aton Villa ipo michezo mingine ya ligi kuu England inayopigwa leo na kesho, ambapo Lawrenson anajaribu kutabiri matokeo.Chanzo BBC

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI