Header Ads Widget

AJALI YAUA WAWILI AKIWEMO MCHUNGAJI



Watu wawili akiwemo mchungaji ambao walikuwa wakielekea harusini wamefariki dunia huku wengine wakijeruhiwa baada  gari waliokuwa wakisafiria kugonganga USO Kwa uso na Lori .

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 asubuhi ya  Novemba 5, 2021 eneo la kata ya Nkininziwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

kamanda wa polisi mkoa wa Tabora A.C.P Richard  Abwao amethibitisha kutokea Kwa ajali hiyo .  

Alisema magari hayo yaligongana uso kwa uso huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa lori aliyehama na kuigonga gari ndogo aina ya Noah.

Kamanda Abwao aliwataka waliofariki kwenye ajali hiyo kuwa ni pamoja na  mchungaji Nathanael Magomola(60) na Recho Msengi (60) wakazi wa Tabora,watatu wamejeruhiwa wanaendelea na matibabu hospitali ya Rufaa Kitete.

Chanzo : CG FmRadio

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI