Header Ads Widget

TGDC KUZALISHA UMEME MEGAWATI 200 (MWe) KUPITIA JOTOARDHI

Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) imesema kulingana na mpango wa Taifa wa uzalishaji umeme wa 2020 (PSMP,2020) imelenga kuzalisha megawati 200 (MWe) na megawati 500 za joto (MWt) zitokanazo na jotoardhi ifikapo mwaka 2025. Mwandishi Fatma Ally MDTV anaripoti toka  Dar es Salaam

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam mapema leo hii na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Katto Kabaka, wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kampuni hiyo, ambapo amesema lengo la Serikali la kuanzisha kampuni hiyo ni pamoja na upatikanaji wa umeme kutokana na vyanzo mbalimbali.

"Dhamira kuu ya Serikali ya kuongeza wigo wa vyanzo vipya vya uzalishaji wa umeme ni kukabiliana na changamoto za sasa za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mahitaji ya umeme kutokana idadi ya watu kukua pamoja na kukidhi matakwa ya sasa ya uchumi wa viwanda na kidigital na mabadiliko ya tabia nchi"amesema Kabaka.


Ameongeza kuwa,Ili kuhakikisha dhana ya joto ardhi na matumizi yake yanatimia, Tanzania kupitia TGDC imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo katika kuendeleza jotoardhi nchini ikiwa ni pamoja na BGR, ARGEO,IGA, NDF na ESMAP.


Hata hivyo, amesema Ili kuendeleza miradi na matumizi ya moja kwa moja ya jotoardhi katika kuchochea ukuaji wa Sekta nyengine mbali na umeme, TGDC inaendelea na miradi ya maonyesho (showcasing) ya uzalishaji wa kuku (hatching) Kilimo cha mboga mboga (geothermal heated greenhouse) pamoja na Burudani na Utalii (geothermal spa).


Ameongeza kuwa, mbali na hayo pia wanaendeleza miradi ya ufugaji samaki (aquaculture ) katika eneo la maji moto Songwe ambapo lengo la miradi hiyo ni kuonyesha jinsi rasilimali ya jotoardhi inavyoweza kuchochea ukuaji wa Sekta nyengine za uchumi na kuonesha fursa za ajira mpya na uwekezaji.

Hata hivyo, amesema mpaka sasa kazi zilizofanyika katika kampuni hiyo, ni pamoja na kukamilisha majaribio ya jotoardhi katika uanguaji na ufugaji wa vifaranga vya kuku kwa kutumia maji ya moto (geoincubator) ambayo inaangua vifaranga kwa  gharama nafuu,pia  kukamilika kwa ujenzi bwawa la kuogelea na burudani la maji moto pamoja na kubuni teknolojia ya kukusanya taarifa za utafiti wa kijiolojia.

Aidha amesema kuwa, mradi huo uliopo Mkoani Songwe unategemewa kuanza na uzalishaji wa umeme (MW 5) na matumizi mengine ya moja kwa moja ambapo gharama za mradi huo ni takriban dola za kimarekani mill 32, huku utekelezaji wa mradi ulianza mwaka 2018 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2023.


Ameongeza kuwa, katika mwaka wa fedha 2021/22 kampuni hiyo inaendelea na utekelezaji kazi ya uchorongoaji wa visima vifupi utafiti (shallow wells) kwa ajili ya kuboresha taarifa zilizopo, kupanua miradi ya moja kwa moja kabla ya kuanza kwa uchorongoaji wa visima virefu vya uhakika (exploratory .




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI