Charles Odero Charles mkurugenzi Cilao
Shirika lisisilo la kiserikali la waandishi wa habari la utetezi wa jamii za pembezoni(MAIPAC) kwa kushirikiana na shirika la ustawi wa wanawake na watoto(WOCWELS) na tasisi ya uraia na msaada wa kisheria (CILAO) wamezindua mradi wa kuwajengea uwezo, uelewa na ujasiri wanawake vijana kutokana tasisi za elimu ya juu ili waweze kupata na kutumia mitandao ya kijamii kudai haki zao za kijamii, kisiasa na kiuchumi.MWANDISHI WA MDTV NAMNYAK KIVUYO ANARIPOTI KUTOKA ARUSHA
Akiongea katika hafla fupi ya kutambulisha mradi huo kwa wanufaika mkurugenzi mtendaji wa tasisi ya uraia na msaada wa kisheria Charles Odero Charles alisema kuwa mradi huo wenye jina DIGITAL LITERACY lengo kubwa ni kujenga au kukuza uelewa na kujenga ujasiri kwa wanawake vijana waliopo katika tasisi za elimu ya juu wafanye nini ili waweze kupata na kutumia nafasi ya digitali katika masuala mazima ya kijamii, demokrasia, siasa na kiuchumi.
“Kama mnavyojua kwa sasa Dunia imehama kutoka analog na kwenda digitali ambapo wengine wameingia kidogo na wengine wapo kasi sana kwahiyo tumekuja na mradi huu mahususi kwa wanawake vijana wenye umri wa miaka 18 Hadi 25 na kwa kuanza tumeanza na chuo kikuu Cha Makumira, Tasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru pamoja na chuo cha mtakatifu Augustino tawi la Arusha,”Alisema Odero.
Alifafanua kuwa katika mradi huo wa miezi mitatu wanatarajia kujenga uelewa kwa wanafunzi namna ambayo wanaweza kutumia mitandao ya kijamii Kama fursa katika masuala ya kijamii, kidemokrasia, kisiasa na kiuchumi ambapo ni jambo muhimu kwani kumekuwepo na malalamiko kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii Ni kupoteza muda au mahali ambapo Kuna uhuni mwingi lakini wao kama mashirika wameona ni vizuri waonyeshe fursa hizo.
Musa Juma Mkurugenzi MAIPAC
Kwaupande wake Musa Juma mkurugenzi wa shirika la MAIPAC alisema kuwa wanataka matumizi makubwa ya tehama kwa wanafunzi kwasababu wanafahamu wanawake wanakabiliwa na changamoto katika jamii hivyo wameona kupitia mitandao ya kijamii wanaweza wakawaunganisha wanafunzi wanawake vijana waliopo katika elimu ya juu ili waweze kutumia mitandao kujiendeleza kielimu.
“Badala ya kutumia hii mitandao kwa vitu ambavyo sio vya maana sana watumie kujiendeleza kielimu, tumeona kuwa hii ni njia rahisi ya siku hizi ya kuwafikia watu wengi na kutoa elimu ni mitandao ya kijamii kwahiyo tumeona tuwasaidie dada zetu ili weweze kutumia kupata ufumbuzi wa masuala mbalimbali yakiwemo ya ukatili wa kijinsia,” Alisema Musa.
Naye Mery Mushi mratibu wa kitaifa wa shirika la ustawi wa wanawake na watoto alieleza kuwa katika mradi huo wamewachukia wasichana kwasababu wameona ni kundi kubwa ambalo limekuwa likidhurika na mitandao ya kijamii kwa Kuna viti vimekuwa vikitokea ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia Kwa mfano video ambazo zinakuwa zinatembea bila matakwa yao .
“Tunataka tujenge ujasiri kwa watoto wa kike lakini pia na wao wajione ni sehemu ya kuleta mabadiliko kwa jamii kupitia mitandao ambapo tunatoa mafunzo kwa wasichana 30 kutoka vyuo vitatu ambao hawa ndio watakuwa mabalozi wa kufikisha elimu hii kwa jamii,”Alisema Mushi.
Mmoja wa wanufaika wa mradi huo Ester Koka kutoka chuo Cha Tumaini alisema kuwa mradi huo utawasaidia kupata nafasi ya kutoa ya moyoni kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanawake vijana ikiwemo udhalilishaji kwa kuweza kupaza sauti zao kupitia mitandao.
0 Comments