Header Ads Widget

PONGEZI KWA FREDERICK NDAHANI-AFISA VIJANA MKOA WA SINGIDA NA MRATIBU WA MBIO ZA MWENGE KWA NGAZI YA MKOA WA SINGIDA


Binafsi niwapongeze Viongozi wa Singida wakiongozwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Binilith Satano Mahenge, Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bi Dorothy Aidan Mwaluko,Wakuu wa Wilaya , wakurugenzi, Viongozi wa Siasa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Chama Tawala(CCM) na wananchi wote wa Mkoa wa Singida kwa kushika nafasi ya Pili (2) Kitaifa katika mashindano ya Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mwaka 2021 na nafasi ya Kwanza (1) kwa kanda namba III, inayojumuisha Mikoa ya Singida,Dodoma, Manyara, Kagera, Mara na Kigoma.


Kwa namna ya kipekee nimupongeze Sana Kaka yangu Frederick Joseph Ndahani Afisa maendeleo Vijana Mkoa wa Singida na Mratibu wa Mwenge wa uhuru Mkoa kwa kazi nzuri ya kuratibu shughuli hii na kuufanya Mkoa upate Matokeo mazuri akishirikiana vizuri na Viongozi wake wa Mkoa,Wilaya, Waratibu wasaidizi, Waratibu wa Wilaya , Viongozi wa vya vya kisiasa na wananchi .


Ndahani ni Kijana anayejituma ,mwaminifu,mchapakazi, mzalendo,mwajibikaji na pia anayeweza kusimamia jambo na likafanikiwa kwa kiwango cha juu na ufanisi.


Nakumbuka Wakati akikimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa aliibeba timu yake vizuri Sanaa licha ya yeye kutokuwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka huo, nakumbuka Kiongozi alikuwa Amour kutoka Zanzibar.


Lakini kwa nafasi yake ya uafisa Vijana Mkoa amewasaidia Vijana wengi wa Mkoa wa Singida na mikoa ya jirani ambapo amewasaidia Vijana kuanzisha miradi,namna ya kusimamia miradi,kuwaungamisha na fursa mbalimbali na Taasisi za kifedha na ujuzi, na juzi ameniambia anaandaa shindano la andiko Bora la mradi kwa Vijana akishirikiana na  Asasi isiyo ya kiserikali inayotwa HELVETAS kupitia mradi ya YESS  ili Vijana waweze kujifunza kuandika maandiko mradi utakao saidia Vijana wa Mkoa wa Singida kuomba mikopo ya 4%,Taasisi za kifedha na wadau wengine.




Mimi nikiwa chuo kikuu cha Dodoma alitusaidia kuanzisha miradi ya kibiashara kwa kutumia fedha tunazo lipwa na Serikali huku tukiendelea na masomo chuoni ,wakati tunasubiri ajira tunaendelea kupata fedha za kujikimu.


Nasema haya kwa kuwa Vijana Sisi hatuna tabia ya kupongezana kwa mazuri tunayofanya katika utumishi, Biashara au masuala ya kijamii.


Nitaendelea kujifunza kwako na Kwa Vijana wengine wanaofanya vizuri katika nafasi zao.


Karibu Mjini Magharibi Kwenye marashi ya karafuu .


By Aziza

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI