Vijana wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI pamoja na mapambano ya matumizi ya Madawa ya Kulevya
Wito huo umetolewa na afisa tawala wilaya ya Morogoro Janneth Chata wakati wa mahafali ya 32 ya chuo Cha Ufundi stadi VETA Kihonda kilichopo Manispaa ya Morogoro
Janneth anasema licha ya taasisi mbalimbali na mashirika ya Umma kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI bado Kuna wimbi kubwa la vijana kujiingiza katika biashara haramu ya kuuza miili yao na kupata VVU.
Anasema Ni wakati wa vijana kufanya mabadiliko kwa jamii kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kipato Cha Taifa na mtu mmoja moja
"Sasa mmekua wasomi nendeni mkafanye kazi za halali ambazo mmesomea ili muwe mfano kwa jamiii bila kusahau kutoa elimu ya VVU ili watu wajue kuwa ugonjwa huo upo na unaua " amesena Janeth
Kwa upande wake mmoja wa wahitimu hao Elizabeth Jerusalem amesema wasichana wengi wanaogopa kusomea fani za ufundi kutokana na uoga na kutojiamini ndomana inaoelekea wengi kujingiza katika biashara ya ngono zembe ili wapate fedha kwa haraka.
Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 210 wamehitimu Kati ya 47 wasichana na 163 wavulana
0 Comments