Prof. Frankwell akizungumza na wanahabari
Maktaba ya mkoa wa Iringa
Na Rehema Abraham Kilimanjaro
Wadau wa maktaba nchini wamekutana mkoani Kilimanjaro katika kongamano la kisayansi la shirikisho la vyuo vikuu na vyuo vya utafiti kujadili namna Bora ya kuboresha na namna ya upatikanaji wa huduma za maktaba na utumiaji wake katika njia ya kidigitali.
Akizungumza katika warsha hiyo Naibu makamu Mkuu wa chuo kikuu Cha ushirika Moshi prof. John Safari amesema warsha hiyo itakwenda kusaidia wanaofanya kazi za maktaba Kama waalimu na na wafunzi wataweza kupata taarifa hizo kwa usahihi.
Kaimu Makamu Mkuu wa chuo kikuu Cha ushirika Moshi profesa John Safari
Amesema kuwa watahakikisha kuwa waalimu na wanafunzi waliopo kwenye nafasi za elimu ngazi ya juu wanatumia makala na maandiko za kitaaluma zilizopo kwenye mfumo wa kidigitali.
"Kwenye upande wa uchapishaji na tafiti mbalimbali taasisi zetu hazijawaa kwenye ngazi Nzuri sana ya kidunia hivyo ninawataka watu wa Tasisi zote za elimu ya juu kufanya jitihada zaidi ya kuhakikisha kuwa wanafanya matangazo kwenye majarida ambayo yanakubalika kidunia ili tuweze kutambulika kidunia kuwa vyuo vikuu vya Tanzania zina sifa Kama vyuo vingine vya Afrika mashariki"Alisema Safari.
Aidha mwenyekiti wa shirikisho Hilo Prof. Frankwell Dule amesema kuwa kongamano Hilo litawajengea uwezo wa kuandika tafiti za kitaaluma na kuwafikia walengwa.
Kwa upande wake Grece msofe mkurugenzi wa huduma za maktaba kutoka Dodoma amesema kuwa machapisho ambayo yapo kwenye njia ya makaratasi na hayawezi kupatikana mtandaoni kompyuta au simu kwa sasa Wana uwezo wa kuchapisha hayo machapisho na kuweka ili kusomeka kwa kutumia dhana mbalimbali za kielektronick.
Hata hivyo Dr Visent Msonge katibu Mkuu wa ( COTUL)shirikisho la maktaba ya vyuo na vyuo vya na vyuo vya utafiti ,na mkurugenzi wa huduma za maktaba katika chuo Cha usimamizi wa fedha amesema kuwa warsha hiyo imelenga kuonesha jukumu la maktaba katika kuwasaidia watafiti nchini kuwa katika ulimwengu wa kidigitali .
"Imekuwa ni changamoto kubwa ndani ya tasisi zetu hasa hapa Tanzania kuonekana machapisho ,kwa hiyo lengo letu kubwa la kufanya haya makongamano Kama hayo ili taarifa zinaweza kuwafikia walengwa "Alisema Msonge.
0 Comments