Header Ads Widget

TANZANIA NA KENYA ZAENDELEA KUJADILI MIKATABA HII

 




Na Teddy Kilanga,MDTV Arusha 

Serikali ya Tanzania na Kenya imeendelea kujadili  na kuweka makubaliano ambayo yatasaidia kukamilisha  mikataba inayotarajiwa kusahiniwa hivi karibuni kati ya nchi hizo ambapo matokeo yake kuongeza ushirikiano.

Akizungumza na waandishi wa habari kando ya mkutano  wa watalam,Afisa Mwandamizi  kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki  ,Paul Makelele alisema lengo la mkutano huo ni kutokana na maelekezo ya ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya katika kujadili mikataba uliofanyika Nairobi mnamo Agasti 20 hadi 24 Mwaka huu

Alisema kupitia mkutano huo ilielekezwa  kwamba kuna baadhi ya mikataba ambayo haijakamilika  katika hutiaji wa saini kati ya nchi hizo mbili  hivyo ilielekezwa kwamba  timu za wataalamu kati ya Tanzania na Kenya wakutane nchini Tanzania kwa ajili ya kukamilisha majadiliano ya mikataba hiyo na ikiwezekana isahiniwe kwa miezi michache inayokuja.


"Mikataba ambayo inajadiliwa ni pamoja na  makubaliano ya masuala ya uhamiaji,mkataba wa kuhusu masuala ya  kupeana wahalifu,kusaidiana katika makosa ya jinai,mabadilisho ya wafungwa kati ya nchi hizo,hati ya makubaliano ya kuhusu masuala ya magereza pamoja na uwekezaji,"alisema Makelele.

Aidha alisema wanatarajia kwamba  majadiliano hayo yatadumu kwa siku tano yatakamilisha makubaliano ya mikataba hiyo ili iweze kusainiwa  kwa miezi michache inayokuja ikiwa katika mkutano huo umewashirikisha wataalamu kutoka  uhamiaji,magereza,wizara ya katiba na sheria,Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serilikali na wizara ya mambo ya nje.

Hata hivyo alisema mkutano huo wa wataalamu umefunguliwa na balozi wa Tanzania nchini Kenya,George Simbachawene pamoja na balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan kazungu unaotarajiwa kufungwa mnamo Novemba 12,2021.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI