Header Ads Widget

UDSM YAADHIMISHA MIAKA 60 KWA KUTOA MISAADA



Na Fatma Ally, MDTV Dar es Salaam


Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kimetoa msaada wa shuka 100 viti mwendo 4 pamoja na vitakasa mikono katika Kituo cha Afya Kimara Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya shukurani kwa jamii tangu kuanzishwa kwa chuo hicho. 


Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof William Anangisye amesema hatua hiyo imekuja ikiwa chuo hicho kimetimiza miaka 60, ambapo maadhimisho hayo yatakuwa endelevu kwa mwaka wote wa masomo kwa kutoa vifaa mbalimbali kwa vituo vya Afya kuanzia Oktoba 25 mwaka huu.



Amesema kuwa, Chuo hicho kimejipanga kuongeza utatifi na ubunifu kupitia pesa za mapato ya ndani, lengo ni kuona chuo hicho kinazidi kukua mwaka hadi mwaka ambapo kumekua na ongezeko la kila mwaka kwa wadahili wanaojiunga na chuo hicho.


"Idadi ya wanafunzi imekua ikiongezeka kwa kasi hadi kufikia 43,307 katika mwaka wa masomo 2020/2021, kati ya hao wanafunzi wa kike ni 19,785 sawa na asilimia 45.7 ya wanafunzi wote ambapo juhudi mbalimbali zimekua zikichukuliwa Ili kuongeza uwiano"amesema  Pro Anangisye.



Aidha, amesema maadhimisho hayo yataendelea kwa mwaka mzima ambapo wataendelea Kutoa vifaa vya kufundishia na maarifa katika shule ya msingi maalum Sinza na kuendelea kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali nchi. 


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amekishukuru chuo hicho kwa msaada huo kwani utawasaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na mahitaji makubwa yaliopo kituoni hapo.



Aidha amesema kwa siku kituo hicho kinahudumia watu wengi hivyo mahitaji ni makubwa kuliko eneo linavyoonekana na kutokana na ufinyu wa eneo ilibidi kijengwe kwa ramani tofauti na vituo vingine.



Hata hivyo amesema Halmashauri ya Ubungo bado inatoa fedha za mapato yake ya ndani kwa ajili ya upanuzi wake na wanasaidiwa pia na TANROAD na TAMISEMI na kikikamilika watahudumia watu wengi zaidi na kuboresha huduma ya Afya kwa jamii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI