Header Ads Widget

MSHUKIWA WA SHAMBULIO LA MISHALE NA UTA AKAMATWA NORWAY

 


Mwanaume mmoja amekamatwa akihusishwa na shambulio la mishale na uta lililotokea nchini Norway .

Na kulikuwa na hofu kuwa alikuwa anaendeleza shambulizi, polisi imesema.

Mwanaume huyo ambaye ana umri wa miaka 37-mwenye uraia wa Denmark anashutumiwa kuua wanawake wanne na mwanaume mmoja siku ya Jumatano huko kusini mwa mji wa Kongsberg.

Kamanda mkuu wa polisi wa Ole Bredrup Saeverud alisema maofisa waliwahi kukutana na mwanaume huyo mwaka jana .

Alikamatwa na kuhojiwa maswali kadhaa majira ya usiku.

Waathirika wa shambulio hilo walikuwa na umri wa kati ya 50 na 70, mkuu wa polisi Saeverud aliwaambia waandishi Alhamisi asubuhi.

Polisi walimkamata mshambuliaji huyo dakika sita baada ya shambulio kutokea siku ya Jumatano lakini alitoroka na kukamatwa tena baada ya dakika 35 baada ya shambulio kutokea.

Polisi wanasema inawezekana watu wote aliowauwa waliuliwa mara baada ya polisi kukabiliana naye mara ya kwanza.Chanzo BBC

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI