Header Ads Widget

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi Tarehe 14.10.2021: Werner, Rudiger, Lang, Coutinho, Tchouameni, Rabiot, Werner, Pedri

 

Wamiliki wapya wa Newcastle Saudia wanapanga kuitegemea Ujerumani katika jaribio la kupata mafanikio ya Jurgen Klopp na Thomas Tuchel katika ligi ya England. Mshambuliaji wa Chelsea Mjerumani Timo Werner, 25, ndiye mchezaji anayelengwa zaidi, pamoja na kiungo mlinda lango wa Bayern Munich na Mjerumani Niklas Sule, 26, Kiungo wa kati wa Barcelona MBrazili Philippe Coutinho, 29, na meneja Mjerumani kama vile meneja wa zamani wa Dortmund Lucien Favre. (Bild - in German)

The Magpies wamewasiliana na wawakilishi wa kiungo mlinda lango wa Ufaransa anayechezea timu ya Leicester City Wesley Fofana kuhusu uwezekano wa uhamisho katika dirisha la uhamisho wa mwezi wa Januari. (RMC Sport - in French)

Kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot amehusishwa na uhamisho wa Newcastle , huku klabu hiyo ya Serie A ikiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mwezi Januari ili kuweza kutafuta fedha za kumnunua kiungo wa kati wa Monaco na raia wa Ufaransa Aurelien Tchouameni au kiungo wa kati wa Manchester United na Uholanzi Donny van de Beek, 24. (Calciomercato - in Italian)

Rabiot

CHANZO CHA PICHA,

Monaco wameweka bei ya euro milioni 60 kwa kijana mwenye umri wa miaka 20 Tchouameni, huku Real Madrid, pamoja na Manchester City, Chelsea na Liverpool wakimtaka mchezaji huyo. (Marca - in Spanish)

Barcelona wako makini kumuachilia Philip Coutinho katika kipindi cha dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku Liverpool ikiwa tayari kumrejesha tena mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 katika uwanja wa Merseyside. (El Chiringuito TV, via Express)

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers ndiiye mtu wa kwanza anayefikiriwa kuchukuliwa na wamiliki wa klabu ya Newcastle iwapo wataamua kumfuta kazi meneja wa sasa Steve Bruce. (Sky Italy via Mirror)

Meneja wa Foxes (Mbweha) Rodgers, hatahivyo, anasemekana ''kujitolea kikamilifu'' kwa klabu hiyo . (Telegraph)

Antonio Rudiger

Real Madrid wanania ya kusaini mkataba na mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger, 28. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani unamalizika mwishoni mwa msimu huu na ataongeza uzoefu wake kwa klabu hiyo ya Uhispania. (Marca in Spanish)

Phil Foden amesitisha mpango wake wa kusaini mkataba na Manchester City wenye thamani ya karibu pauni milioni 50, huku makubaliano ya kiungo huyo ya miaka sita yakimuwezesha kulipwa pauni 150,000 kila wiki (Mirror)

Arsenal wanajianda kwa dau la euro milioni 30 kwa ajili ya winga wa klabu ya Club Bruges mwenye umri wa miaka 22 Mholanzi Noa Lang. (Voetbal24 - in Dutch)

Joules Kounde

CHANZO CHA PICHA

Manchester United wanaweza kufufua juhudi zao za kusaini mkataba na kiungo mlinda lango wa Sevilla Mfaransa Jules Kounde ambaye pia bado analengwa na Chelsea . (Fichajes, via FourFourTwo)

Barcelona wamepiga hatua katika mazungumzo yao na kiungo wa kati wa Uhispania Pedri kuhusu mkataba mpya, na kiungo huyo wa miaka 18- yuko tayari kukubali mkataba ambao utaendelea hadi 2026. (Goal)

Mlinzi wa Borussia Dortmund na Ujerumani Mats Hummels, 32, amemuonya Erling Braut Haaland, 21, kwamba huenda "asipate mazuri'' akiondoka klabu hiyo. Manchester City, Manchester United, Chelsea na Real Madrid wote Wanataka kumsaini mshambuliaji huyo wa Norway. (Bild - in German)

Erling Braut Halaand

CHANZO CHA PICHA

Paris St-Germain huenda wakamnunua mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu. PSG, hata hivyo inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Tottenham, Juventus na Bayern Munich kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia wa miaka 21. (Le 10 Sport - in French)

Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone alijaribu kumsajili Lionel Messi, 34, msimu wa joto na ametoa maelezo ya jinsi alivyompatia kibarua hicho mshambuliaji Luis Suarez kumshawishi mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona kujiunga na klabu hiyo kabla aamue kuhamia Paris St-Germain. (Ole, via Mail:Chanzo BBC

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI