Header Ads Widget

MLIPUKO WA BANDARI YA BEIRUT:WAFYATULIANA RISASI KATIKA MAANDAMANO YA KUPINGA UCHUNGUZI WA MLIPUKO HUO

Takriban watu sita wameuawa na wengine 32 kujeruhiwa na risasi katika mji mkuu wa Beirut nchini Lebanon.
Yote haya yalianza wakati wa maandamano yaliofanywa na makundi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia , Hezbollah na Amal dhidi ya jaji mmoja aliyekuwa akichunguza mlipuko mkubwa mwaka jana katika mji huo wa bandari.

Walisema kwamba wanajeshi wa kuvizia wa dini ya Kikristo kutoka kwa jeshi la Lebanon LF walifyatua risasi katika kundi moja la watu kwa lengo la kuishinikiza Lebanon kuingia katika ghasia - madai yanayopingwa na jeshi hilo.

Hali ya wasiwasi inazunguka uchunguzi uliosababisha mlipuko huo uliowaua watu 219. Wapiganaji wa Hezbollah na washiriki wake wanadai kwamba jaji huyo anapendelea, lakini familia za waathiriwa wanaunga mkono kazi yake. Hakuna hata mtu mmoja ambaye amepatikana na hatia ya mlipuko huo wa Agosti 2020, ambapo maeneo mengi ya mji huo yaliharibiwa vibaya.

Akijibu mashambulizi ya siku ya Alhamisi , ambayo yameonekana kuwa mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni, waziri mkuu Najib Mikati alitangaza siku ya kuomboleza siku ya Ijumaa.

''Hatutaruhusu mtu yeyote kuliteka nyara taifa hili kwa maslahi yao ya kibinafsi'' Alisema Rais Michel Aoun.


Kile kilichoanza kama maandamano nje ya kasri la haki - jengo kuu la mahakama - ambapo mamia ya wakaazi walikuwa wakikosoa uchunguzi huo -kilishinikizwa kisiasa na kuwataka raia kutaka jaji huyo Tarek Bitar kuondolewa, kulingana na mwandishi wa BBC Anna Foster mjini Beirut.

Ufyatulianaji wa risasi ulizuka katika barabara za mji huo wakati kundi hilo la watu lilipokuwa likivuka mzunguko wa barabara katika eneo la katikati mwa mji la Tayouneh- Badaro.

Wakazi walilazimika kutoroka makazi yao huku wanafunzi wakikimbilia maeneo ya kujificha chini ya madawati yao huku watu waliokuwa wamejihami na bunduki pamoja na magurunedi , wanaoaminika kuwa wanachama wa dhehebu la Shia pamoja na Wakristo walipofyatuliana risasi barabarani.

Ghasia ziliendelea kwa saa kadhaa kabla ya utulivu kurudi.

Katika shule moja, walimu waliwaagiza watoto kulala wakiangalia chini ardhini huku mikono yao ikiwa kichwani , shahidi mmoja alikimbia chombo cha habari cha Reuters.

Chanzo; BBC Swahili.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI