Header Ads Widget

MLIPUKO WAUKUMBA MSIKITI WA AFGHANISTAN WAKATI WA IBADA

Wengi wahofiwa kufariki baada ya mlipuko kutokea katika msikiti wa dhehebu la Shia wakati wa ibada ya Ijumaa katika mji wa Kandahar Afghanistan .

Vyombo vya habari vinaripoti kwamba mlipuko huo ulitokea katika msikiti wa Imamu Bargash na kwamba idadi kubwa ya watu wameuawa.

Hatahivyo chanzo cha mlipuko huo hakijatajwa licha ya kwamba kuna tuhuma za mlipuaji wa kujitolea muhanga. Kundi la wapiganaji wa Taliban liliteka mji wa Kandahar, mji wa pili kwa ukubwa nchini Afghanistan tarehe 13 Agosti baada ya vita vikali.

Chanzo; BBC Swahili

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI