Na, Titus Mwombeki-MDTV BUKOBA.
Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Kagera wamesema wapiti kipindi kigumu cha kusafirisha bidhaa kutoka mkoani humo kwenda mkoa wa Mwanza kutokana na meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU kusitisha safari zake kwaajiri ya kufanyiwa matengenezo.
Akizungumza na Matukio Daima TV Amri Athuman mfanya biashara wa ndizi, palachichi pamoja na ndizi kutoka Bukoba kwenda Mwanza alisema kutokana na kukosekana kwa meli hiyo imewaingiza kwenye gharama kubwa.
“ Kukosekana kwa meli hii imepelekea sisi kama wafanyabiashara kutumia gharama kubwa kusafirisha bidhaa zetu kutoka Kagera kwenda Mwanza kwani tumekuwa tukitumia usafiri wa maroli ambavyo ukiangalia gharama zake nikubwa ukilinganisha na gharama za meli katika sualazima la usafirishaji”.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa safari za meli hiyo inayofanya safari zake kati ya Bukoba na Mwanza itarejea rasmi Octor 15 mwaka huu.
“Meli ya NEW MV VICTORIA hapa kazi tu iliyositisha safari zake kwaajiri ya kufanyiwa matengenezo Octoba 15 kwaka huu itaanza safari zake kama kawaida”. Amesema Mbuge.
Ikumbukwe kuwa, meli ya NEW MV VICTORIA HAPA KAZI TU ilisitisha safari zake mnamo tarehe 27 septemba mwaka huu.
1 Comments
🙏🙏🙏🙏
ReplyDelete