Header Ads Widget

TARI KIHINGA YAHAMASISHA UPANDAJI WA MBEGU MPYA YA CHIKICHI AINA YA TENERA

 


Na mwandishi wetu, Kigoma. 


Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania TARI Kihinga iliyoko mkoani Kigoma Dkt. Filson Kagimbo anasema kuwa Tanzania tuna aina tatu za chikichi ambapo zipo za kienyeji dula(jiwe) inapatikana kwa asilimia 90 na pisifera(bubu) inapatikana kwa uchache chini ya silimia 0.01  hii ya kisasa ambayo inaitwa tenera(hote) ambayo inapatikana kwa asilimia 9.9 hizi ni aina tatu ambazo zinapatikana duniani kote.


Anasema kuwa uzaaji wa  zao la chikichi aina ya dula ambayo inatoa mafuta kidogo wastani wa 1.6 kwa hekta ambapo aina ya pisifera haipatikani kwa urahisi na haikamuliwi mafuta lakini pia ni chache sana unaweza kuwa na shamba la hekali moja lakini ukakosa mti hata mmoja wa bubu.


Anasema kuwa aina ya mbegu ya Tenera inapatikana kwa asilimia 9.9 ambapo ukilima unapata tani 4-5 kwa hekta  ndio maana serikali inahamasisha wakulima kutumia mbegu hiyo ambayo imeonyesha kuwa msaada mkubwa katika utatuzi wa uhaba wa mafuta nchini.


“Kwanini tunasema kuwa ni mbegu bora tunaangali vitu viwili ukipanda Tenera inaanza kuzaa baada ya muda mfupi yaani baada ya miaka miwili hadi mitatu unaanza kuvuna tofauti na dulla ambayo ukipadna unaanza kuvuna baada ya miaka 5-7 ndio maana tunaiita bora” alisema Dk Kagimbo


“Ukitaka kulima kwa tija inakubidi ulime tenera ambayo ndio inaweza kuongeza na kukuza uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla kwa sasa tunalima eneo la mchickichi hekta 30,000 ambayo tunapata tani 40,000 za mafuta uwezo wetu kwa mazao yote ni tani 240,000" 


Na kuongeza "ukiangalia mchikichi mchango wake wake unaonekana ni mdogo ndio maana tunalenga kuongeza mafuta kwakutumia mchikichi kwkauw ni zao ambalo linaaminika duniani kwakutoa mafuta mengi”


“Mfano ukilima alizeti hekta moja unapata tani 0.8 ukilinganisha na mchikichi utaona jinsi gani inazidi alizeti kwa upatikanaji wa mafuta ndio maana serikali imeona iwekeze kwenye zao hili ambapo asilimia zaidi ya 80 inatokana”


“Tanzania kwa mwaka 640,000 mafuta ya kula sisi tunaliza asilimia 37 tu ndio tunazalisha ili upate zote kwenye mchinikichi inabidi ulime hekta 150,000 ambapo utahitaji miche milioni 20,000 ili upade eneo lote tumeanza kuzalisha ambapo tumezalisha miche milioni 7265 tutahitaji miaka 3”


“Tukifanikiwa tutakuwa tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini kumbuka yapo mazao mengine yanayotoa mafuta pia ambayo ni pamba, ufuta, karanga na alizeti”


“Kwa magonjwa yote yanafanana kwasababu aina hii mpya tumechavusha kutoka kwenye aina dula na pisifera ndio maana zinafanana kwa tabia na kushambuliwa na wadudu na magonjwa”


“Bei ya chikichi imetofautiana kulingana na msimu ambapo kuanzia mwezi wa tisa hadi wa tatu mavuno yanakuwa mengi na bei zinakuwa nafuu huuza lita kwa 1500 lakini wakati ambao sio wa msimu huuzwa 2000 lakini baada ya serikali kuhamasisha uhamasishaji wa michiukichi bei imepanda hadi kufikia shilingi 3000”


“Unajua haya mafuta ya safi, korie, mukwano yote ni mafuta ya mawese lakin wengi hawajui na yana bei kubwa sana kuliko mafuta yenyewe ya asilia” alisema Dk Kagimbo


Nae Mkurugenzi wa uhaurishaji teknolojia na mahusiano kutoka tari Juliana Mwakasendo alisema kuwa taasisi hiyo imekuwa na kazi kubwa ni kuhakikisha kuwa tunatoa teknolojia zote zilizo na watafiti wetu na kuzifikisha kwa watumiaji.


Sisi tunahakikisha kuwa teknolojia zote tunazitoa kwenye makabati na kuzipeleka kwa watumiaji kwanni tunazipelkeka tumeona tija ni ndogo kwenye mazao mbalimbali tunapopeleka tija tunaona maboresho katika kilimo


Viwanda vingi asilimia 65 wanatumia mazao sisi kama tari lazima tutumie fursa zilizopo nchini ili kuhakikisha kuwa wadau mbalimbali wamepata elimu stahiki ili kuweza kunufaika kwenye mnyororo wa thamani


“Sio tu wadau tuna vituo nane ambavyo vinatumika kwaajili ya kutolea elimu kwa wakulima mbalimbali kwa mwaka mzima  hata hivyo kupitia vyombo vya habari vipeperushi mbalimbali tunaweza kutoa elimu mbalimbali” alisema Mwakasendo


Nae Tatu Ramadhani mkulima wa zao la chikichi wilayani kigoma anasema kuwa serikali imeonyesha nia ya kuwasaidia katika kuinua zao la chikichi hivyo wanaamini kuwa wataweza kufanya mambo makubwa zaidi kwenye zao hilo.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI