Header Ads Widget

MUHIMBILI, PINKY LEGACY INITIATIVE WAUNGANA KUHAMASISHA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI


Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Pinky Legacy Initiative wameandaa shughuli ya ustawi wa afya katika Grand Waves, ikiwa sehemu ya kuadhimisha Mwezi wa Uhamasishaji wa Saratani ya Matiti, kwa lengo la kutoa elimu na kuwapa moyo mashujaa wa saratani ya matiti.

Akizungumza katika shughuli hiyo, Daktari Bingwa wa Saratani wa MNH, Dkt. Sara Nyagabona, amesisitiza umuhimu wa kutambua dalili za saratani ya matiti mapema, kufanya uchunguzi na kuwahi hospitalini kwa matibabu stahiki. Pia ameeleza umuhimu wa elimu katika kupunguza hofu na dhana potofu kuhusu ugonjwa huo.

Shughuli hiyo imewakutanisha mashujaa wa saratani ya matiti kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kutiana moyo na kuimarisha mshikamano katika kukabiliana na ugonjwa huo ambapo MNH na Pinky Legacy Initiative zimeendelea kuhamasisha jamii kufanya uchunguzi wa mapema na kutafuta matibabu kwa wakati, huku zikiitaka jamii kuwaunga mkono wagonjwa wa saratani ya matiti.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI