Urusi imeshambulia vituo sita vya nishati vya Ukraine saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kwamba nchi hizo mbili zimekubaliana kusitisha mapigano ya nishati, Volodymyr Zelensky amesema.
Licha ya Trump kusema Jumapili kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yataanza "kutekelezwa mara moja", rais wa Ukraine alisema Urusi imeshambulia "vituo vyetu vya mafuta, miundombinu ya nishati, na vifaa vingine".
Kulikuwa na kukatika kwa umeme katika jiji la Izyum baada ya mashambulizi ya Urusi kuharibu mitambo ya umeme, shirika la habari la serikali la Ukraine Ukrinform lilisema, huku miundombinu ya nishati na reli magharibi mwa Ukraine pia vikilengwa na mashambulizi usiku kucha.






0 Comments