Header Ads Widget

JESCA KITAMBAA CHEUPE AZINDUA CHIMBO LA VIJANA BRUNCH 2026

 

Na Matukio DaimaMedia 

Mfanyabiashara na Mjasiriamali Jessica Boniface Kikumbi, maarufu kama Jesca Kitambaa Cheupe, amezindua hafla ya Chimbo la Vijana Brunch 2026, inayotarajiwa kufanyika Oktoba 24 na 25 katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijjni Dar es Salaam, Jesca, ambae ni mmiliki wa kumbi za burudani na baa za Kitambaa Cheupe nchini Tanzania, amesema hafla hiyo inalenga kuwaunganisha vijana na wananchi katika jukwaa moja litakalowawezesha kupata huduma za kijamii, burudani na elimu kuhusu ajira, kodi, uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi.


Amesema hafla hiyo itashirikisha taasisi mbalimbali zikiwemo Bodi ya Mikopo, TRA, Idara ya Uhamiaji, RITA, Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani, taasisi za bima, watoa huduma za afya na taasisi za uwekezaji. Taasisi hizo zitatoa elimu na ufafanuzi kuhusu huduma zao, taratibu za kuzifikia na fursa zilizopo.


Aidha, washiriki watapata burudani kutoka kwa ma-DJ na wasanii mbalimbali katika siku zote mbili, pamoja na huduma ya supu ya bure kuanzia asubuhi.


Kwa mujibu wa Jesca, hafla hiyo inalenga kupunguza muda na gharama za wananchi katika kutafuta huduma sehemu tofauti, huku ikiwapa vijana nafasi ya kuuliza maswali, kubadilishana mawazo na kupata taarifa zitakazowasaidia kuendeleza shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI