![]() |
| Tuzo ya mshindi wa Uhusiano Bora na Vyombo vya Habari Tanzania 2026 (Best Media Relations in Tanzania 2026) aliyoshimda TMDA, 9, Oktoba. |
Dodoma:
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeendelea kung'ara katika sekta ya mawasiliano baada ya kunyakua tuzo ya mshindi wa Uhusiano Bora na Vyombo vya Habari Tanzania 2026 (Best Media Relations in Tanzania 2026)
Tuzo hizo zimetolewa jana 8 Oktoba, 2026 katika hafla ya utoaji tuzo za Umahiri wa Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano (PR & Communications Awards ) iliyoandaliwa na Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST).
Tuzo hizo ni kielelezo cha umahiri wa taasisi hiyo katika matumizi ya vyombo vya habari kufikisha elimu sahihi kwa umma kuhusu masuala ya dawa na vifaa tiba na kuongeza chachu ya kuendelea kudumisha weledi na ufanisi katika mawasiliano ya umma.
Tuzo hizo, hutolewa kila mwaka na PRST kwa kupigiwa kura na wadau mbalimbali.







0 Comments