Header Ads Widget

SINTOFAHAMU KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU KUKUTWA JIRANI NA OFISI YA KATA YA ISAKALILO



SINTOFAHAMU imejitokeza katika mtaa wa Njiapanda kata ya Isakalilo Manispaa ya Iringa baada ya wananchi kukuta box lenye kiganja cha mkono wa binadamu ndani. 

Matukio Daima Media imefika eneo la tukio na kuzungumza na mashuhuda ambao wamedai kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 7 mchana wa leo Jumapili September 27/2026.


walisema kuwa kata hiyo imekuwa ikikumbwa na matukio ya ajabu ajabu na kuwa hawajui mhusika wa tukio hilo ni nani hasa. 

Hata hivyo walisema kutokana na sintofahamu hiyo walilazimika kujulisha uongozi wa serikali ya mtaa na kata pia polisi kata kwa hatua zaidi.


Mwenyeki wa serikali ya mtaa huo Maisha Modestus Kihuko alisema kuwa alipigiwa simu majira ya saa 6 mchana na baada ya kufika alikuta mkono huo ukiwa na ujumbe wenye kurasa sita ambapo moja moja kata ya jumbe hizo kuwa "Mkono huu ufike Iringa"

Alisema tukio hilo kama linahusishwa na Imani za kishirikina ndani yake Ila vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi zaidi. 

TAZAMA VIDEO YA TUKIO BONYEZA HAPA

Hata hivyo askari polisi waliofika eneo la tukio waliomba wananchi kutoa ushirikiano na pindi watakapobaini mtu hana mkono ama mhusika wa tukio hilo basi wasisite kutoa taarifa polisi

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI